Jun 21, 2011

SAUT MWANZA SURUALI MARUFUKU

Chuo kiku cha Mt.Augustine University of Tanzania (SAUT) main campus- Mwanza kimepiga marufuku wanawake kuvaa suruali. Hatua ya kupiga marufuku uvaaji wa mavazi hayo kumetokana sura mbaya inayotokana na uvaaji wa suruali,kwani zimekuwa za kuwabana hivyo kusababisha maumbile kuwa wazi na kuwafanya kuonekana kama makahaba. Wakazi wengi wa Nyegezi kilipo chuo pamoja na wanafunzi wa kiume wamepongeza uamuzi huo kwani ilikuwa ni kero kubwa. Chakushangaza ni kuwa watu ambao ni wasomi wanaotegemewa kuliongoza taifa kwa nyanja mbalimbali ndio wanaoonekana kuvunja maadili ya kitanzania. Katikati ya jiji ukiona binti amevaa nguo mbaya hasa visuruali na kimkoba ujue ni mwanafunzi wa SAUT. Kutoka chanzo cha kuaminika kutoka chuoni hapo zinasema kunawanafunzi wachache ambao walikaidi walitimuliwa.Wasichana wote waliokuwa sugu kwa uvaaji wa hovyo wameuponda uamuzi huo na kuonesha kutokukufurahia lakini hawana namna hasa katika kipindi hiki cha mitihani ya mwisho wa semester ya pili kwani hawaruhusiwi kuingia na suruali hivyo kulazimika kuingia dukani kununua sketi. Vituko kwa akinadada hao baadhi vimeonekana kwa kuamua kuvaa sketi nyepesi ambapo mtu amaweza kuona aibu zingine. Mwisho mi ninajiuliza,hivi elimu si ndio inayokufanya mtu uheshimike? Mbona sasa wenye elimu za juu ndio wanaofanya vituko? Mwanamke lazima aongozwe na sio aachiwe kujitawala.Naomba vyuo vingine viige mfano huu wa SAUT ili kulinda hadhi ya mwanamke na hadhi ya Tanzania pia.

May 1, 2011

FORUM MPYA!

Wiki hii forum mpya kwa waislam na hata wasio waislam imeanzishwa .Anuani yake ni www.islam.freeforums.org "Jukwaa la waungwana".Watu wote wanakaribishwa kuandika habari maalum za kiislam,siasa,ndoa,sayansi,elimu,ushairi na mengine mengi.Unachopaswa kufanya ni kujiandikisha ili kupata uwezo wa kuandika na kujibu post mbalimbali.Baada ya ujumbe huu wewe ni balozi wa kuitangaza habari hii ya kuanzishwa kwa forum.Wote mnakaribishwa www.islam.freeforums.org "Jukwaa la Waungwana".

Apr 26, 2011

KWA SIRI HII, MUUNGANO HAUVUNJIKI NG'O!

Leo tarehe 26 tunasherehekea miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe rasmi zinaadhimishwa katika uwanja wa Amani Zanzibar na mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho kikwete. Mengi yanasemwa kuhusu huu muungano wa Jamhuri ya Tanzania lakini wengi wao wanakwepa kuusema ule ukweli unaotakiwa kusemwa. Naomba ni mnukuu Mh.mama Anna Komu alipokuwa anahojiwa na TBC1 "wananchi wa Zanzibar hawakushilikishwa wakati wa kufanya muungano,ila walikaa viongozi na kukubaliana".Wazanzibar wamelalamika siku nyingi juu ya Muungano huu hadi ukazuka msamiati wa "kero za Muungano".Zimeundwa kamati mbalimbali kushughulikia muungano lakini bado kamati hizi bado hatujaona matunda yake kwa maana ya kuziondosha kero za muungano. Je,Muungano waweza kuvunjika? Jibu lake ni HAPANA. Kwanza nianzie nyuma kidogo ili nikuoneshe ni kwanini Muungano hata kwa dawa hauvunjiki yaani hata Wazanzibar walie machozi ya damu. Tanganyika ilitawaliwa awamu ya kwanza na Wajerumani kisha wakaja Waingereza,nyakati zote hizi wazee wetu walipambana kudai uhuru wa Tanganyika na hatimaye mwaka 1961 uhuru ukapatikana.Wakati wa mbio za kudai uhuru Mwl.Nyerere ndiye pewa jukumu na wazee ili aende kwenye Jumba la mabwanyenye akadai uhuru. Maombi ya uhuru yakakubaliwa chini ya masharti.Masharti hayo kwenye mkataba ambao ulikuwa siri kati ya nchi tawaliwa na watawala,hadi sasa hakuna ajuaye Mwl.Nyerere alisaini masharti gani ili tupewe uhuru ambayo yeye alikubaliana nayo.Baada ya uhuru Mwl.Nyerere alitia fitina na kuuvunja umoja wa Waislam Afrika Mashariki(EAMWAS) na kuwafukuza mashekhe nchini na wengine kuwaweka kizuizini.Baada ya kuivunja EAMWAS aliwaundia Waislam BAKWATA ilikuwa chini ya uangalizi wa serikali yake. Hapa nia na madhumuni ilikuwa kuwavunja nguvu Waislam,kwa kuwa tayari walikuwa na nguvu kubwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii.Hivyo waislam waligawanywa na wakagawanyika pia nguvu ikaisha kwa kuwa mashekhe walifukuzwa nchina na wengine kizuizini, hivyo harakati za uislam kusonga mbele zikafifia na mahala pengine kufa kabisa,hii ilitokana na hofu kubwa waliyokuwa nayo wanaharakati baada ya kushuhudia yaliyotokea kwa ndugu zao. Kwa upande wa Zanzibar,Zanzibar yenyewe ilitawaliwa na Sultan kutoka Oman pia baada yake walitawala watoto wake mpaka pale waingereza walipo kuja kuleta fitna baina ya watawala ambao ni watoto wa Sultan.Waingereza walimpatia silaha mtoto mmoja wa Sultan ili apambane na nduguye juu ya madaraka ya kuitawala Zanzibar,baada ya mapambano aliyekuwa madarakani alikimbia na kumwachia mshindi ambaye ni kibaraka wa Waingereza. Kipindi chote cha utawala wa Sultan hadi kwa watoto wake wote wawili Uislam Zanzibar ulinawili na kuwa na nguvu kubwa.Uislam ulikuwa umeenea maeneo yote ya pwani na kuanza kuingia bara kwa kasi.Baada ya uhuru wa Zanzibar mchakato wa muungano ulianza haraka sana ambapo 1964 Tanzania ilizaliwa.Agenda kuu ya siri ilikuwa kuudhibiti Uislam usienee bara kwa nguvu kwani EAMWAS ilikuwa tayari imekufa. Mambo yote ya muungano huamuliwa Dodoma,Zanzibar ikawa inachaguliwa marafiki tena wale ambao Dodoma iliwataka. Kumbuka Zanzibar ilipotaka kujiunga na OIC haraka Dodoma ilikataa na kusema hilo ni jambo la muungano na Zanzibar sio nchi na madai hayo ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano. Hofu iliyopo nikuwa Zanzibar ikijitenga Uislam utapata nguvu na kuhatarisha ustawi wa Ukristo Afrika mashariki hivyo lazima Zanzibar idhibitiwe kwa vyovyote vile hata kama wananchi hawataki.Wote waliohoji muungano hawakosalama na mifano tunaiona wazi,Abdu Jumbe alihoji,akaitwa Dodoma na kuvuliwa nyadhifa zake zote na kuishia kizuizini na historia yake ikafutika.CUF na sera yao ya "tukipata madaraka tunavunja muungano" wakatiwa lupango kina Duni Haji na kupewa kesi ya uhaini. Pia inasemekana kuwa hata Karume aliuawa baada ya kuazimia kuvunja Muungano baada ya kujua siri iliyopo. Wazanzibar sasa wanalilia muungano kuvunjika na hili limedhibitika hivi karibuni ambapo wananchi walichanachana muswada wa katiba mpya ambao haukutaka Muungano kujadiliwa,kutokutaka muungano kujadiliwa kuna maana kuwa mambo yalivyo yaendelee kuwa hivyohivyo na asiyetaka ashughulikiwe. Ustawi wa ukristo nchini unategemea nguvu ya Uislam nchini kwani mambo yanayotokea hivisasa yanadhibitisha. Kumbuka uchaguzi wa mwaka2000 ambapo ilikuwa dhahiri CUF Zanzibar ilishinda ila kutokana na sera yake ya kuuvunja muungano CUF ikakosa madaraka na kuwalazimu wananchi wa Zanzibar kuingia barabarani ambapo walisagwasagwa kwa mkono wa chuma,mauaji makubwa yalitokea na kwa mujibu wa DotchWelle idhaa ya kiswahili ambapo mwanamke mmoja alikuwa akihojiwa na kwa uchungu alisema "huko mtaani maiti zimezagaa,kwakusia watu zaidi ya 80 wamekufa,kwani askari wanapiga risasi hovyo na kunawengine wanawekwa kwenye makarandinga.Na kunahabari kuwa kuna mashua ilikuwa na raia wakikimbilia Kenya wamefuatwa kwa helkopta na kupigwa kombora". Hata hivyo habari za helkopta zilikanushwa.Kwa siri hii kuu,Muungano hauvunjiki ng'o!

Apr 24, 2011

PASAKA NA UNAFIKI WA AMANI

Amani ni kitu cha muhimu sana,yaani katika ngazi tofauti au ngazi mbalimbali kuanzia mtu binafsi,familia na taifa kwa ujumla.Kila mmoja wetu kama binadamu hupenda kuishi kwa amani bila kukwaruzwa kwa jambo lolote.Tatizo lililopo kwenye amani ni unafiki wa baadhi ya wanadamu ambapo wao huipenda amani na kujivunia kwayo lakini wao hawapendi wengine kuishi katika amani na pia hufurahi wanapoona jirani hana amani,watu hawa pia hutafuta nafasi za kuchokonoa amani za wengine hivyo kuleta kutokuelewana na hatimaye amani kupotea kabisa. Wiki hii tumeshuhudia na wengine kushiriki katika ibada na mikesha ya pasaka ambapo hotuba juu ya amani zilitawala. Kweli ilikuwa ni muhimu kwa mahubiri hayo kutawaliwa na kilio cha amani kutokana na umuhimu wa amani lakini,kwanini amani inaonekana kutoweka nchini? Je,ni kinanani wako nyuma ya moto huu mbaya? Je,ni viongozi wa dini au wa kisiasa? Jibu ni kuwa viongozi wa dini wenyewe na pia kwa kuwatumia wanasiasa ndio wamekuwa chanzo cha mvurugiko wa amani.Kama nchi ina makundi katika jamii na hasa moja likapewa nguvu na jingine kunyanyaswa! Hapo amani karibu ipo kutoweka. Viashiria vya kuvunjika amani Tanzania vipo wazi kabisa na vipo katika mtazamo wa kisiasa zaidi kwa wale wasiotambua,lakini mtafaruku huu uko wazi kuwa ni wakidini japo wasioona watapinga kwa nguvu. Kwa mfuatiliaji wa mambo yeye tayari ameng'amua mapema dalili zote.Vita iliyopo sio ya ccm na chadema bali ya Waislam na wakristo kwa sura ya kisiasa zaidi. Ndugu msomaji utakubaliana namimi kuwa makongamano ya Waislam yamefunua dhulma nyingi dhidi ya Waislam na hadi kulalamikiwa kuwa ni hatari eti kwasababu yanaelezea halihalisi ya Waislam nchini. Imefikia hatua vyombo vya habari vya Waislam kutishiwa kufungwa hasa gazeti la An-nur na radio Imani inayotangaza kutokea mjini Morogoro. Matusi na kejeli kutoka kwa vyombo vya habari hasa magazeti ambayo mengi yanamilikiwa na wakristo imekuwa ni kawaida,pia mtandao wa jamiiforum umekuwa chanzo cha kusambaza sumu ya udini nchini na mgawanyiko wa itikadi. Lengo langu kuu ni kuzitazama hotuba za pasaka kwa ujumla,lakini hebu tukumbuke nyuma kidogo ambapo mauaji ya Mwembechai,Zanzibar na Arusha na tulinganishe halafu tazama mwenendo wa katiba mpya kisha chukua hamasa za chadema kwa wananchi na wanafunzi wa elimu ya juu kisha uone.Rudi nyuma tazama mjadala wa mahakama ya kadhi Tanzania na lile la Tanzania kujiunga na OIC ambapo vitu hivi vilisababisha viongozi wa kidini kusema "damu itamwagika endapo serikali itaiingiza nchi OIC na kuwapa mahakama za kadhi Waislam".Mwerevu anajua na kutambua hatari tuliyonayo inatokea upande gani.Kumbuka tena vurugu za Arusha ambapo viongozi wa chadema walisema "tutahakikisha nchi haitawaliki".Maneno haya ni mazito sana! Lakini je,viongozi wa dini waliyagusia kwa uzito wake? Au walirashiarashia? Dr.Wilbroad Peter Slaa yeye ni Padri na kuingia katika siasa hizi yeye na chama chake wana agenda ya siri! Na hili hakuna kiongozi wa dini yeyote anayeweza kulizungumzia kwani huyu ni mwakilishi wao,badala ya kumkemea wao wanamtetea! Sasa kilio cha hotuba za pasaka kuhusu amani ni Unafiki mtupu kwani wahubiri wanajua tatizo lilipo na hawaoni haja ya kulitatua kwa malengo yao wanayoyajua. Hotuba au mahubiri na yaliyonyoyoni mwa wahubiri ni vitu viwili tofauti kabisa. Twende Rwanda kwenye mauaji ya kimbali,kule nako ilikuwa kama kwetu ambapo kwenye ibada tunahubiriwa amani na upendo lakini mwisho wa siku wahubiri ndio walikuwa washiriki wakubwa wa mauaji ya kimbali(halaiki) nchini humo. Kama kweli hotuba hizo zina dhamira ya kweli kutaka amani ya nchi basi wangeomba viongozi wa dini wote wawekwe pamoja na serikali na pia wale wakisiasa wakalishwe chini ili nyufa zizibwe la sivyo tutaishia kwenye dimbwi la damu. Ama kwa hakika kanisa na viongozi wake ndio wanao hatarisha amani yetu kwa kuandika nyaraka za kuligawa taifa kwa misingi ya dini,mfano mzuri ni nyaraka za kuelekea uchaguzi ambapo nyaraka hizo ziliandaliwa ili wakristo wamchague mgombea aliye chaguo la kanisa,kweli hii ni hatari sana! Kama wao ndio wanaoshabikia vitendo vya uvunjifu wa amani basi kweli msisitizo wa amani ni UNAFIKI uliowazi tena ni unafiki mweupe usio na doa. Napenda nichukue nafasi hii kumkumbusha Rais Jakaya M. Kikwete juu ya ahadi ya kukutana na viongozi wa dini mara kwa mara kwani huu ndio wakati muafaka ambapo nchi inatetemeka kabla ya kuanguka na kuvunjika vipandevipande.

Apr 10, 2011

TAIFA KUMOMONYOKA.

Taifa la Tanzania lina viashilia vyote vya kumomonyoka mfano wa mmomonyoko wa udongo(landslide). Kwanza kabisa ni Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ambao ndio unaounda jamhuri ya Tanzania nao umeonesha kulegea kutokana na Wazanzibari hawauhitaji muungano kwa madai ya kutengwa kwenye mambo muhimu ya kitaifa.Hivi majuzi baada ya serikali kuandika muswada wa katiba huko Zanzibar katika majadiliano ilishuhudiwa wananchi wakisema wazi kuwa muungano hawautaki ikiwa nipamoja na kuchanachana muswada wa katiba hadharani huku waziri wa Afrika mashariki Mh.Samwel Sitta akinusurika kupewa kipigo.Pili katika makongamano ya katiba imeonekana kuwa kuna makundi yaliyoandaliwa nawanasiasa ili kuzomea wale wenye mawazo tofauti na wao pia na viashilia vya uvunjifu wa amani ulio wazi katika maeneo hayo.Vuguvugu la maandamano ya chama cha CHADEMA kuwa ndio chachu ya taifa kutokuwa katika utulivu wake kutokana na vijana kuwa na mihemko mikali ya kiitikadi ikihamasishwa na viongozi wao wa chama.Kwa muswada wa katiba ambao unaonekana haukidhi mahitaji ya wananchi huu pia imekuwa chanzo kipya cha nchi kutokutulia.Tatu,kama katiba itatengenezwa baada ya maoni yanayoendelea kutolewa,katiba hiyo haitapitishwa na wananchi kwani itaendelea kutokujali maeneo mengi ya wananchi ambapo raia iko wazi wataandamana kupinga katiba hiyo nchi nzima na polisi endapo watayazuia basi maafa makubwa yakatokea.Nne,hata kama kaiba ikakubalika kwa baadhi ya vipengele na kuletwa kwa wananchi, kundi jamii la kiislam halitapitisha katiba hiyo kama haijarudisha mahakama ya kadhi na hivyo kuzua maandamano na makongamano ambayo huenda yakazuiwa na polisi na hivyo kuleta maafa,upande wapili wa wakristo ambao umekuwa wameonesha upinzani wa hali ya juukwa haki hii ya Waislam kupewa haki hii ya kuabudu,hivyo endapo katiba itakuwa na mahakama ya kadhi basi wakristo wataleta vurugu na maandano nchini ambapo Waislam Watawakabili kwa kila namna ili kutetea na kulinda haki hiyo na hapo maafa makubwa kutarajiwa kwa kuwa wakristo maranyingi wamekuwa wakiingilia haki za waislam kwa kutumia bunge na watendaji ambao ni wakristo,kutokana na dhuluma hii iliyokuwepo Tanzania muda mrefu basi hapo itaonesha ni kiasi gani Waislam wamekasirishwa na tabia za wakristo na hapa vita vya kidini kuwa ndio mwanzo.Endapo mapigano ya kidini yatazuka basi na jeshi la polisi litagawanyika kwa misingi ya kiimani na hivyo kushindwa kuleta amani.CHADEMA ambayo inatajwa wazi kuwa na agenda za dini ya kikristo na kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la vijana pia kinatajwa kutaka madaraka kwa nguvu kwa madai ya kura zao kuchakachuliwa hivyo kutumia mwanya wa vurugu za kidini kupora madaraka ya nchi.Kama jeshi la Tanzania halitaingilia kati wakati huo basi taifa litakuwa limeangamia.Siasa za chuki miongoni vyama na wafuasi wao ambapo hapo juu nimetabanaisha kuwa chadema wanatajwa kuungwa mkono na wakristo pia ccm ikitajwa kuwa rafiki wa waislam, hivyo mapambano kati ya vyama hivi mwisho ni vita vya kidini kutokana na uungaji nkono hivyo taifa litakuwa na makundi makuu mawili yanayopambana. Amani tuliyojivunia miaka mingi basi huenda ikatoweka tusipokuwa makini na tusipo pendana na kupeana haki.Tuitunze amani yetu.

Apr 7, 2011

WAKRISTO ACHENI POROJO LETENI HOJA.

Kutokana na makongamano ya Waislam yanayoendelea nchini hivi sasa zimeletwa hoja nyingi sana juu ya makongamano hayo. Wakristo wameonesha kuguswa sana na makongamano hayo na kuamua kuanza kuzungumza chinichini na hadi kutaka mamlaka ichukue hatua.Malalamiko makubwa ya wakristo ni kuwa makongamano, gazeti la An-nuur na radio hasa Radio Imani kuwa vinaleta uchochezi! Swali: Uchochezi ni nini? Je,kuna jambo ambalo waislam wanaongopa? Kama lipo na litajwe wazi.Haki haiombwi lakini inachukuliwa Je, mnataka waislam waanze kwa kuichukua haki yao,badala ya kuiomba kwa amani? Ni ukweli uliowazi kuwa ndugu zangu wakristo hawana hoja juu ya MFUMO KRISTO ambao upo kuhakikisha waislam na uislam haupigi hatua kwenda mbele. Nyaraka nyingi na vitabu vilivyo andikwa na wasomi wa Kikristo ndio ushahidi wa yale yanayofanywa na kanisa dhidi ya Uislam.Kuna madhila mengi tu ambayo waislam wamekumbana nayo tangu uhuru hadi leo.Waislam ni wapenda amani na kama sivyo basi tusingeshirikiana kwa lolote katika jamii.Hoja za kusema waislam wanaleta uchochezi huku ni kukosa hoja juu ya yale yote yaliyotajwa katika makongamano.Udini unaooneshwa na wakristo ni mkubwa sana na ndio maana hata Mufti alilisemea kwa kutoa agizo kwa waislam kuwa sasa inatosha Waislam kuwa kimya na sasa wazungumze.Waislam wanapopanda majukwaani huja na hoja za kweli zenye ushahidi wa wazi.Hivi? Mtu akikukanyaga si lazima useme? Sasa waislam baada ya kimya wameamua kuzungumza! Hivyo wakristo leteni hoja zenye mantiki juu ya MoU,Mfumo Kristo na upotoshaji wa historia ya Tanganyika na wala sio kusema tu eti uchochezi.Leteni hoja zenye mantiki na ushahidi na msikalie kusema eti hao hawakusoma.Hivi maaskofu waliposema damu itamwagika na waislam wanosema tupeni haki ni nani mchochezi? Kumbuka kuwa kila inapozuka hoja yenye maslahi kwa Waislam hupata upinzani mkali sana kutoka kwa Wakristo,mfano mzuri ni hoja iliyopelekwa bungeni na Waziri wa elimu Mh.Prof.J.Kapuya miaka ya tisini iliyohusu sala ya Ijumaa na Hijjab.Waziri alipigwa madogo na vijembe na wabunge walio wengi ambao niwakristo.Tukija hoja ya OIC na mahakama ya kadhi sote tumelishudia lililotokea nchini ambapo waandishi waliandika na maaskofu wakasema na kukemea haki ya Waislam, jamani hadi hapo nani hataki amani? Hapa siwezi kuorodhesha mambo yote hapa kwani ni mengi na mifano hai iko mingi tu.Kama kweli wakristo wanaona wanaonewa juu ya shutuma toka kwa waislam basi na wasimame viongozi wajibu hoja juu ya hoja na sio kuleta porojo za uchochezi. Waislam na wakristo sote twapenda amani lakini kama wakristo wameichoka amani basi wao waanze japo tayari wameshaanza na waislam watamaliza.HAKI NA USAWA NI KWA WOTE KATIKA NCHI HII NA SI KWA KUNDI MOJA TU.Pia kumbuka thamani ya kitu huwezi kuijua hadi ukipoteze ndio utatambua uthamani wake,hivyo wakristo wakae na wajenge hoja zenye mshiko na sio kuleta porojo.

Mar 26, 2011

WIMBO HUU TBCtaifa HAPANA.

Wimbo wimbo unaotumiwa kama kidokezo cha hotuba za hayati Mwl.Nyeree TBCtaifa kwakweli ni upotoshaji mkubwa wa historia ya Tanganyika.Muda mrefu wimbo huu nimekuwa nikiutathmini na kuutafakari na kukosa majibu kwa siku nyingi lakini sasa hatimaye nimegundua kisa na mkasa wa haya yote. Wimbo unasema "...kama sio juhudi zako Nyerere na uhuru tungepata wapi...? Kama sio juhudi zako Nyerere na amani tungepata wapi...?" Hii ni sehemu ya wimbo huo na mashairi yake ndio yaliyosababisha leo niseme haya nitakayosema.1.Watunzi wa wimbo huu na walioleta wazo la wimbo na wapigaji wa wimbo wanalengo la kuipoteza historia yote ya wapigania uhuru na kuonesha kuwa juhudi zote na kazi yote ya uhuru kafanya nyerere pekee. 2.Lengo ni kuonesha kuwa Nyerere ndio mwasisi wa mwanzo na wa mwisho wa harakati za kupigania uhuru na kuonesha au kukiaminisha kizazi kipya na kijacho kuwa Nyerere ndiye shujaa pekee katika historia ya Tanganyika.3. Wale wote waliojitolea kwa mali zao pia kumpa dhamana Nyerere kuwa kiongozi katika chama ambacho hakukianzisha na ambacho kilikuwa na malengo wala hawatajwi wala kupewa sifa na kuthaminiwa kuwa ni watu muhimu katika historia ya nchi yetu.Vitabu vya historia pia vyafuata mkumbo huohuo wa kumsifu Nyerere.4.Wimbo huu unaopigwa TBCtaifa usimamishwe maramoja na kutafutwa wimbo au kutafutwa kidokezo mbadala ambacho kinawatambua au kutambua juhudi za waasisi wa harakati za uhuru.Kupindishwa kwa historia ya Tanganyika ni juhudi za makusudi za kundi fulani kutaka kuonesha kuwa kundi jingine halina mchango wala halikuwa na mchango wowote katika mbio za kusaka uhuru.Kumbuka kuwa wakati wengine wakihudhuria ibada pamoja na wakoloni kundi la pili lilihangaika kuusaka uhuru wa nchi hii. Kundi hilo lililokula sahani moja na wakoloni leo linaeneza chuki za kidini kwa kueneza nyaraka za siri kwenye nyumba za ibada.Wakati kundi moja likidharauliwa kundi jingine linajineemesha na mikataba mbalimbali pia kupata misaada. Naomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya watu wachache wenye tabia hii mbaya ambayo muda si mrefu italiangamiza taifa.Serikali iandae majina halisi ya wapambanaji wa harakati za uhuru wote pasipo kumbagua yeyote miongoni mwao.Historia sahihi ya Tanganyika iandikwe kwani kuna uongo mwingi unaowekwa au uliowekwa kwenye historia na mfano mdogo ni kama wimbo huu wa wosia wa mwl.Nyerere kwenye redio ya Taifa. Kizazi kijacho hakitaijua historia na mashujaa kwa kuwa hawatajwi hata maramoja na hata serikali nayo iko kimya. Kweli wimbo huu ni mwiba kwa historia na kizazi kipya hakitawajua mashujaa bali Nyerere pekee.

Mar 21, 2011

DR.KIKWETE JIBU HOJA YA DR.SLAA.

Dr.Slaa mara kwa mara amekuwa akimtaja Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete katika kashfa za ufisadi. Katika ile the list of shame Rais kikwete alitajwa,na kutajwa huku kunatajwa hadharani kweupe lakini Rais Kikwete alijibu tu kuwa yeye si mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans. Rais Kikwete amehusishwa pia na Kagoda ambayo imevuna mabilioni ya mipesa katika akauti ya madeni ya nje ya EPA. Dr.Slaa amekuwa na kiburi cha kusema na kutaja kwa ujasiri mkubwa sana majukwaani, lakini hadi sasa hajafikishwa mahakamani kama alivyoburuzwa Mchungaji Christopher Mtikila alipo mdhihaki Rais. Hoja kuu iliyopo hapa ili kuondoa wasiwasi kwetu sisi raia tunataka Dr.Wilbrod Slaa afikishwe mahakamani kwa kumhusisha Rais na ufisadi.Kushindwa kumpeleka au kumshtaki Dr.Slaa inamaanisha ni kweli Dr.Slaa anao ushahidi wa wazi juu ya vitendo vya ufisadi kwa Rais Kikwete. Sasa hamu na shauku yetu wananchi ni kuona mahakama inatikisika kwa Dr.Slaa kufikishwa mahakamani. Ukimya wa mamlaka ya nchi kukaa kimya inatupa wasiwasi sana na kuamini kuwa yote yasemwayo ni kweli.Mwisho,nasisitiza tena na tena Dr.Slaa afikishwe mahakamani, na hoja zake pia zijibiwe kuliko kukaa kimya.

Mar 18, 2011

ASKOFU RWUA'ICHI UMETUDANGANYA.

Askofu wa jimbo la Mwanza ndugu Rwua'ichi jana alikana kanisa Katoliki kukiunga mkono chama cha CHADEMA wakati akihojiwa na shirika la utangazaji Tanzania TBC1. Askofu alisema kuwa wakatoliki wako katika kila chama,hivyo yeye anashangazwa na habari hizo za kanisa lake kukiunga mkono CHADEMA. Hakika siasa zinazoendelea katika nchi yetu ni mbaya sana na hatua makusudi zisipochukuliwa basi umoja na amani ya Tanzania itatoweka na kuirejesha itakuwa tabu.Nataka kumuonesha Askofu jinsi ambavyo hakusema kweli, na sio rahisi kwa yeyote hata Kardinali Pengo hawezi kulikili hili hata siku moja.Mara nyingi hutokea na kukanwa mambo yanapobainika mfano kuna vitabu vilikuwa sokoni vikaondolewa baada ya kubainika vina mikakati ya siri ambayo mingine imetekelezwa na mingine ikitarajiwa. Askofu ametudanganya wapi? Hebu na akumbuke waraka wa Kardinali Pengo wa miaka ya 90 ambao tunaamini ndio ulio sababisha mauaji ya Mwembechai.Kwani kwenye waraka huo Pengo analalamikia mihadhara na umoja wa waislam kuwa ni hatari kwa Ukristo Tanzania na baadae likaibuka kundi la Wakristo waliosomeshwa Qur'an na matokeo yake au adhali zake ni kama zile za Mto wa Mbu kule Arusha, japo haitajaripotiwa lakini hata Mwanza ugomvi uliwahi kutokea mwaka 2010 miezi ya mwanzo pale kwenye viwanja vya mbugani palipokuwa panafanyika mdahalo kati ya waislam na wakristo na baadhi kuumia kidogo.Askofu Rwua'chi ni wazi hawezi kusema hadharani juu ya kukiunga mkono chama cha chadema, kwani wakati wa uchaguzi zilitolewa nyaraka kwa makanisa yote ili wakristo wote wachague chadema.Waraka huo wa mwisho kabla ya uchaguzi ulitoa tahadhali kwa wakristo hasa viongozi kuwa waraka huo ni kwaajili ya viongozi tu na muumini wa kawaida haruhusiwi kuuona ispokuwa kazi kubwa itakuwa kufikisha ujumbe kwa njia ya mahubiri. CCM na CUF ni vyama vya waislam hivyo tukichague chama chetu cha chadema ilisema sehemu ya waraka huo kwa makanisa.Uungaji mkono wa kanisa ni kwa chadema umedhihilika Mkoni Rukwa ambako waumini walioonekana kukiunga mkono chama cha CCM walifukuzwa ushirika. Rukwa ni mbali nami, lakini chuki kwa wakristo chuki kubwa imepandikizwa juu ya waislam na viongozi wenye majina ya kiislam.Haya nayajua kutokana nakuwa naishi na wakristo na mengi huzungumzwa, asilimia tisini ya watu nifanyao nao kazi muda wote ni wakristo na inapoibuka mijadala ya wazi wao pia hujipambanua na hata kusema waliyoelekezwa kutenda. Kwahaya mimi naamini askofu hakusema kweli kwani halihalisi inajionesha wazi.Kuna wale wanaoamini kua magazeti hayasomwi na wengi lakini ukweli wa magazeti sikuhizi umebadilika kwani watunasoma magazeti mtandaoni na mengine kuchambuliwa redioni, na baadhi ya magazeti yana chochea uvunjifu wa amani na kuligawa taifa, hasa kwa kuwaaminisha wasomaji kuwa Viongozi wote wakuu ambao ni waislam hawanatija kwa Taifa na hawajui uongozi.Mpaka sasa nchi imegawanyika, rejea makala yangu ya nyuma isemayo "ya misri hayawezekani tanzania".Kanisa linao wajibu wa kuhubiri amani na upendo makanisani kwani chuki juu ya waislam iko wazi,asiamini na ajaribu kuingia Jamiiforums.com na aone vile post zinazohusu waislam au uislam zilivyo chafu au akae na kikundi chochote cha wakristo na asikilize mada juu ya waislam na uislam,utaona jinsi chuki ilivyo. Utagundua kuwa hakuna mkristo yoyote ambaye anashirikiana na wakristo hata kama ni kwa kiwango cha chini ni shabiki mfuasi mkubwa wa chadema,hii pia ni dalili ya wazi kuwa hilo linajadiliwa kwenye sehemu za ibada. Hebu jamani tuilee na kuitunza amani yetu na tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa.

Mar 17, 2011

PESA ZA BANDIA ZA KAMATWA MWANZA.

Kaimu kamanda mkuu wa jeshi la polisi ndugu Deusdedith Msemeki akitoa taarifa za pesa chafu kwenyemzunguko wa fedha.Kamanda huyo alisema kiasi cha shilingi za kitanzania milioni kumi na nane lakisita na hamsini na tano elufu ambazo zimekusanywa kutoka maeneo mbalimbali. Akiendelea kutoa taarifa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na pesa hizo za bandia kwani zenyewe ni nene kidogo kuliko zile noti halali.Njia nyingine ya kuzitambua ni kuwa hata kama ni mpya noti bandia huchoka kwa kupauka haraka sana, na endapo pesa hizi ziko kwenye mabulungutu(bundles) zina tabia ya kufanana namba, kama ni AB......99 au 100 basi noti karibu zote zitafanana namba hizo.Pia kamanda ameelezea kuwa pesa hizi husambazwa kwa kufikishwa kwenye maeneo ya watu wengi kama minadani,sokoni,kwenye magari hasa daladala na hata benki pia.Hivyo aliwataka wananchi kuwa makini na fedha za bandia bila kuwataja watengenezaji na wasambazaji au kuwa wametiwa mbaroni au la.Hata hivyo amesema wanashughulika na pia kuzijulisha mamlaka kwa hatua zaidi.Mawazo yangu binafsi ni kuwa kama imewezekana kwa noti halali kurudufiwa kwa wingi ambapo hili limekuwa tatizo tangu pale tu pesa mpya zilipoingia tu kwenye mzunguko ni vema serikali ingeziondoa pesa hizi mpya kwenye mzunguko wa fedha. Kwakuwa pesa mpya ni rahisi sana kutengenezwa na watu wasio waaminifu, pesa hizi ziondolewe na zile za zamani ziendelee.Kwani kuacha mtindo huu kuendelea kutauangusha kabisa uchumi wetu kwa kuwa na mipesa mingi sana kwenye mzunguko ambapo hata kamanda amekiri kuwa benki pia pesa chafu hupita kwa mabeki teller wasio waaminifu.

PINDA OMBA MSAMAHA KWA MAGUFULI!

Wiki chache zilizopita waziri mkuu Mh.Pinda alipokuwa ziarani mkoani Kagera alitoa kauli ya kumdhalilisha waziri wa barabara Mh.Magufuli.Kauli ya Mh.Pinda ilikuwa ya kusitisha bomoabomoa kwenye hifadhi ya barabara kuu sanjari na matangazo makubwa ya biashara,ambapo hii ilikuwa ni kauli ya kitendaji ya waziri mwenye dhamana. Kama mh.Pinda aliona ni vyema zoezi hili kusitishwa ni bora angewasiliana na waziri husika na kukubaliana kwanza,kuliko kusimama hadharani na kutoa maamuzi kama hayo.Hadi sasa kuna tetesi kuwa waziri Magufuli ameandika barua ya kujiudhuru wadhifa wake huo kwa Rais Kikwete.Kama ni kweli basi upepo wa kisiasa utabadilika tena baada ya kutulia kwa muda na hasa baada ya kuibuka kwa suala la dawa ya kuponya magonjwa sugu kule Loliondo. Kweli hata mimi binafsi ninajisikia vibaya sana kwa uamuzi huu kwani kwamfano hapa Mwanza mabango yote makubwa yalikuwa yamebanduliwa na kusubiri tu kung'olewa kwa kuwa tayari yalikuwa na alama ya 'x' lakini cha kushangaza baada ya amri hiyo ya Magufuli mabango yale yamebandikwa tena,huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na hata kama ni mimi waziri ningejiudhuru.Ili kuondoa ombwe hili mapema Mh.Pinda aombe radhi kwa Mh.Magufuli.

Mar 6, 2011

'AU' YAPATA HASARA SOMALIA.

Majeshi ya African Uniun yanayoisaidia serikali dhaifu ya Somalia yamepata hasara kubwa baada ya kupoteza wanajeshi wapatao themanini.Majeshi hayo yanayoundwa na wanajeshi wengi kutoka Uganda na Rwanda yamekuwa Somalia kwa muda sasa ili kuipa serikali nguvu.lkumbukwe kuwa Somalia ilikuwa kwenye vita vya kikoo kwa muda mrefu hadi pale ilipoundwa serikali ya mpito ambayo ilikuwa ikifanyia shughuli zake nchini Kenya.Yote haya ni kuwa mabwana wa vita walitetemesha nchi hiyo na vikosi vingi vilivyotumwa huko vilishindwa.Baada ya umoja wa mataifa kushindwa kuleta amani nchini Somalia,kikaibuka kikundi cha kiislam ambacho kilitangaza Jihad dhidi ya mabwana wa kivita.Hatimaye mabwana wa vita walishindwa vita na Somalia kuwa yenye amani ambapo iliundwa serikali chini ya mahakama za kiislam na Amani kudumu kwa miezi sita.Mahakama hizi ziliweza kudhibiti hali ya amani ya nchi hadi pale Ethiopia ilipoingilia kati na kuishambulia Somalia wakiungwa mkono na wamarekani kwa kupewa vifaa na makomandoo ili kuiangamiza amani chini ya mahakama za kiislam mnamo mwaka 2006.Waziri mkuu wa Ethiopia Meresy Zenawi aliishambulia Somalia kwa kisingizio chakuwa mahakama za kiislam zinataka kutawala hadi Ethiopia,ikawa chanzo kipya cha mapigano nchini Somalia.Mapigano yalikuwa makali hadi majeshi ya kiislam yalipoamua kuondoka mjini kwa kuwa raia wengi walikuwa wanakufa.Vijana wa Kisomali waliamua kujiunga na kuunda kikundi chenye nguvu cha Al-shabab ambacho hadi sasa kiko kwenye mapambano makali na majeshi ya AU.Hivyo hii iko wazi kuwa umoja wa mataifa na umoja wa Afrika umeshindwa kuleta amani nchini somalia.Laiti kama mahakama za kiislam zingeliendelea kuidhibiti nchi basi amani Somalia ingekuwepo hadi leo kwani waliweza kudhibiti nidhamu.Wamarekani walichangia kwa madai ya kuwa ugaidi utatia mizizi pembe ya Afrika.Visingizio hivi ndivyo hadi leo vinasababisha hakuna amani pembe ya Afrika.

Mar 3, 2011

CHADEMA FUTENI KAULI YENU.

Kauli ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ya hivi karibuni jijini Mwanza huenda yakazua hatari kwa nchi na uvunjifu wa amani.Kauli hiyo ambayo ilikuwa kuwahamasisha mamia ya waandamanaji waliokuwa wamefulika katika uwanja wa Furahisha kwa kuwauliza kama wako tayari kwa maandamano kama ya Misri na Tunisia na kazi hii ikifanywa na mwenyekiti wa chama Mh.Freeman Mbowe "mkotayari kuandamana kama Misri na Tunisia?" watu wakaitika "tuko tayariii!" na haya yakifanyika maratatu ili kuhakikisha kama kweli watu wameridhia.Kama katika mikutano yote ya CHADEMA itakuwa hivi basi matarajio ni kuwa baada ya hapo huenda chama kikatoa tamko la maandamano nchi nzima,baada ya kazi ya kuwahamasisha raia.Endapo yatafanyika maandamano hayo ya kuipinga na kuifukuza serikali madarakani huenda yakaleta maafa kwa raia kwani sidhani kama serikali itakubaliana na hali hiyo.Vurugu zitasababisha uchumi kuparanganyika na watakaoumia zaidi ni watu wa hali za chini zaidi,kwani biashara ndogondogo hazitakuwepo na uharibifu wa mali kutokea.Vurugu zitakapoendelea watu watauana kutokana na visa tofautitofauti na kisingizio cha vurugu za kisiasa kutumika. Hadi sasa vijana wamehamasika kwa kiasi kikubwa sana, na hii ni kwasababu hawajui madhara ya vurugu.Mfano wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana baada ya vurugu zilizofanyika jijini Mwanza ambazo zilidhibitiwa mapema, baadhi ya vijana walisikika wakilalamika kuwa "hawa polisi wangesubiri giza liingie" nikajiuliza walitaka kufanya nini? lakini wakati huo ofisi ndogo za ccm zinaungua moto pale Nela.Kama wakati ule hakukuwa na kauli ya kiongozi wa chama aliyetamka kuwa tupinge matokeo na madhara yakaonekana vipi leo? Kauli hii ya chadema kwa sasa imekuwa mjadala wa nchi baada ya Rais Kikwete kulihutubia taifa na kuwaonya chadema kuacha kuhamasisha vurugu. Kwa kuwa katiba inaruhusu kuandamana basi chadema waandamane lakini si kuhamasisha vurugu na uvunjaji wa amani. Kilamtu amepewa uhuru na katiba wa kuongea na kutoa maoni yake lakini si kuvunja amani.Ombi langu kwa chadema,futeni kauli yenu ya kufanya maandamano ya kuifukuza serikali madarakani, kwani mpaka sasa wananchi wamegawanyika mapande mapande na wakati huohuo suala la udini likiwagawa raia,basi futeni kauli yenu na mwendeleze hoja za msingi ambazo zitatuunganisha Watanzania pamoja ili tuupige vita ufisadi kwa nguvu moja,kwani fisadi hana dini wala chama.

Feb 28, 2011

VITA WAISLAM NA WAKRISTO VYANUKIA.

Tabia ya kutoa kashfa kwa dini zingine huenda ikaangamiza umoja wa kitaifa.Wakristo Mjini Magharibi Zanzibar wameendeleza chokochoko dhidi ya wenyeji wao ambao ni waislam. Wakristo hao wanatoa kashfa kwa Waislam na Uislam kwa kumtukana Mungu na mtume Muhammad. Mbaya zaidi kama hawajaridhika waliamaua kukidhalilisha kitabu kitakatitifu cha Qur'an kwa kukichoma moto.Waislam walivumilia na kuamua kuzijulisha mamlaka husika pia na kuamua kumwandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.Lakini pamoja na juhudi hizo hakuna hatua madhubuti zozo zilizochukuliwa hadi sasa.Kutokana na hilo la wakristo kuachwa wakiudhalilisha Uislam,Waislam kwa kauli moja wameamua kutokulalamika tena bali nikuchukua hatua ya kuwaadabisha wafanyaji wa vitendo hivyo.Endapo wakristo wataendele basi vita kali huenda ikaripotiwa na hasara kubwa kutokea.Chokochoko hizi za kidini huenda zikaumong'onyoa kabisa muungano wa Tanzania,na tabia hii isipozuiliwa huenda ikaumong'onyoa umoja miongoni mwa raia na kusababisha maafa na kutoweka kwa amani nchini,kwani bado tuna kumbukumbu ya yale yaliyokea Mto wa Mbu kule Monduli mkoani Arusha. Serikali inatakiwa kuyafanyia kazi malalamiko ya kidini yote yanayo wasilishwa kwao kwani inaonekana kuna uzembe ama kutokujali. Hatua zisipochukuliwa Taifa huenda likatumbukia kwenye vita ya kidini na kuliangamiza Taifa kwani dalili ndio hizi.

Feb 27, 2011

MABOMU YALIPUKA SHINYANGA

Mabomu yaliyolipuliwa na jeshi Mkoani Shinyanga yamezua hofu. Hofu hizo zimetokana na wananchi ama kwa kupuuza au kutokuwa na taarifa sahihi,kwani jeshi lilikuwa tayari limetoa tangazo.Tangazo hilo kwa wananchi liliwafahamisha raia kuwa kutakuwa na ulipuaji wa mabomu. Maeneo ya Kizumbi ndio hasa yaliyokuwa kwenye hofu kubwa baada ya milio mizito kusikika.Baadhi ya wananchi walianza kukimbia ili kujìhami. Wengi walidhani yale ya Mbagala na Gongo la Mboto yamehamia Shinyanga. Baada ya ulipuaji huo hakuna maafa yaliyoripotiwa,kwani katika hofu mengi hujitokeza.WITO, Jeshi lihakikishe linasambaza taarifa kwa watu kwa muda mrefu kabla ya shughuli nzito kama hizi ili kuondoa hofu au hata maafa yasiyotarajiwa,kwani inaonesha watu wa Shinyanga hawakuwa na taarifa. Hata kule Gongo la Mboto taarifa zilitolewa mapema kuwa kuna kila dalili ya kulipuka mabomu ila inaonesha wachache ndio waliopata taarifa hizo,hivyo basi maafisa habari wa jeshi wanatakiwa kuhakikisha kwa njia zote taarifa zinawafikia wananchi.

ZIJUE SABABU ZA WATU KUTOKUPIGA KURA 2010.

Uchaguzi mkuu wa Tanzania wa oktoba 2010 ulikumbwa na tatizo la uchache wa wapiga kura. Sababu zipo nyingi zilizo sababisha uchache huo. 1. Baadhi ya wananchi kutokuwa na imani na viongozi wanaowachagua kwa madai ya kujijali wao wenyewe na kuwasahau wapiga kura wao.Hivyo wananchi hawakuona haja ya kwenda kupiga kura kwa kuwa wanaamini wanasiasa huomba kura kwa hoja nzuri lakini baadae huangalia matumbo yao "siwezi kupoteza muda wangu kwenda kupiga kura ili kumpa mtu ulaji akashibishe tumbo lake na familia yake,sina haja! Yoyote atakayeshinda kwangu sawa tu" haya ni maneno ya mwananchi mmoja aliye kubali kuwa hakupiga kura. 2. Baadhi walijiandisha na kupata vitambulisho kwa nia ya kuwasaidia katika mambo yao binafsi,mfano,kusajili namba zao za simu na kubwa ni kwa ajili ya kuchukulia mikopo katika taasisi za fedha na sababu zingine kwa kuwa hadi sasa hakuna vitambulisho vya kitaifa. 3. Taarifa zingine zinasema kuna baadhi ya wagombea walinunua vitambulisho vya kupigia kura na hasa vitambulisho vya wanaoonekana huenda wakawapa kura zao wapinzani wa wagombea hao.Kiukweli hili lilikuwa likituhumiwa sana kuwa ndio chanzo cha kupunguza idadi ya wapiga kura. 4. Uzembe wa baadhi ya wapiga kura wa kutokwenda kutazama majina yao kabla ya siku ya kupiga kura na ambapo kuna majina hayakuonekana kwenye kituo cha kupigia kura.Ambapo walitakiwa kwenda kabla kutazama majina yao na kama hayaonekani au yamekosewa walitakiwa kutoa taarifa ili marekebisho yafanyike. 5. Tume ya uchaguzi kushindwa kuhakikisha hakuna mwananchi aliye rukwa kwa kutazama na kulinganisha orodha kabla ya kuchapa na kutuma vituoni, hapa inaonesha kuna uzembe na kutokujali ambako kumesababisha baadhi ya wananchi pamoja na kuwa na vitambulisho kukosa haki yao ya kupiga kura. 6. Wananchi baadhi walikuwa wagonjwa siku hiyo pamoja na kupewa kipaumbele wanapofika katika vituo lakini wengi wao hawakwenda.7.Hofu ya kutokea machafuko na uvunjifu wa amani katika vituo nayo pia ilikuwa sababu ya baadhi kutokwenda kupiga kura. 8. Kukosekana kwa elimu ya uraia kwa baadhi ya wananchi ambao waliona hakuna umuhimu wa kupiga kura na wengine hata kusema"kura yangu moja haipunguzi wala kuongeza chochote" ambapo walisahau ule usemi usemao " kidogokidogo hujaza kibaba". Hizi ndizo sababu mimi nilizoziona,kwa ushauri wangu katika uchaguzi mkuu wa 2015 mianya hii izibwe ili wananchi wengi waweze kujitokeza kwa wingi kupiga kura,mfano suala la elimu ya uraia litiliwe mkazo sana. Wagombea wanaotoa rushwa na hongo ili kushinda, wakidhibitika wachukuliwe hatua kali ikiwa ni pamoja na kufutiwa haki ya kuwa mgombea maisha.

Feb 26, 2011

UDINI WA KIKWETE NI UPI?

Siasa za Tanzania zimetumbukiwa na nyongo tena nyongo kali. Nyongo hii ni Udini uliotawala ndani ya nyoyo za Watanzania, maranyingi nimesikia kuwa Rais Kikwete mdini na anawapendelea Waislam.Basi na tutazame na mwisho tuangalie huo udini uko wapi.Katika matamko kadhaa ya Waislam inaonesha kweli kunatatizo kubwa nchini mwetu. 2005 Kikwete alikuwa chaguo la Mungu kwa makanisa na maaskofu,wakristo kweli walimkubali,waislam nao walikubali baada ya kuahidiwa mahakama ya kadhi,mahakama ambayo itahusu mambo ya kiislam kama ndoa na mirathi. Baada ya ushindi wa Kikwete ilifuatiwa na uteuzi wa baraza la mawaziri.Baada ya uteuzi huo wiki chache baadae likazuka jambo na magazeti yakaandika kwenye kurasa za mbele. Kikwete ajaza waislam,baraza latawaliwa na waislam-hivi ni baadhi tu ya vichwa vya habari kwenye kurasa za mbele. Ikagundulika kuwa tatizo ni vitu viwili tu,navyo ni kardinali kuondolewa kwenye baraza la mawaziri, swali la kujiuliza alikuwa anaingia kwenye baraza kama nani? Hili likawakera maaskofu. Pili,kuondolewa kwa ubalozi wa papa Ikulu,swali ubalozi wa papa unangoja nini Ikulu na una mwakilisha nani na kwasababu zipi? Baada ya Kikwete kuhoji uhalali na kuondoa vitu hivi akawa adui mkubwa na kuwa si chaguo la Mungu tena mwaka 2010 na hata baadhi ya waumini wa kanisa kule Rukwa kufukuzwa kanisani na kufutiwa ushirika kwasababu tu walimpigia kura Kikwete. Kuibuka kwa hoja ya waislam kuipeleka Tanzania OIC na kurejeshewa waislam mahakama ya kadhi,vikao vilikaliwa na hata baadhi ya wachungaji na maaskofu kufikia hatua ya kusema 'damu itamwagika,endapo waislam watapewa mahakama na OIC'. Hivyo mpaka hapo utajua mdini ni nani! Ikulu ni ya Watanzania wote,baraza la mawaziri ni kwa ajili ya mawaziri wateule tu. Hoja na chuki zikapandikizwa miongoni mwa wakristo ili Kikwete awe sio kiongozi anayefaa,kwani tayari mambo na misheni za kanisa zinaonekana kuingiliwa. Kikwete akaitwa na anaitwa mdini na hafai kuongoza Taifa hili.Labda nikumbushe tu kuwa wakati Rais yeyote Muislam anapoongoza nchii basi atakumbana na hali ngumu kisiasa hata afanye mazuri hayaonekani na yeye huitwa asiye na akili. Mpaka hapo mdini ni nani? Turejee kampeni za uchaguzi wa Oktoba mwaka jana,ambapo udini ulionekana wazi japo wengine waliukana japo nyuso zao zinasomeka. Nchi hii niyetu sote Waislam na Wakristo basi na tuheshimiane ili kudumisha amani yetu. Mmoja mwenye nguvu amehodhi vitu vingi na yule dhaifu ana kidogo,anapotokea wakutaka kuweka angalau kupunguza tatizo basi mwenyenguvu huona anataka kupokonywa vyote hivyo mapambano hapo huanza. Udini udini upo sana lakini kwanini? Kigezo elimu? Hapana kwa kuwa sasa jamii karibu yote sasa inasaka elimu kwa nguvu. Sina ugomvi na dini yoyote,lakini hili ni tatizo.Mfano tulikuwa na jamaa zangu nikawaambia kwa hali ya siasa za Tanzania sasa CCM inahali ngumu 2015 labda wampitishe mtu anayekubalika kama Dr.Salim,wakang'aka yaani Muislam tena? Tumechoka! Nikagundua kumbe ni kweli mambo haya! Mahala popote panapokuwa na kiongozi wa juu Muislam huonekana hana uwezo na nafasi hiyo amepewa kwa upendeleo.Tabia hii ni mbaya. Niwazi kuwa kwa hayo yote ccm haiwezi kua chaguo bora kwa baadhi ya ndugu zangu. Niwazi kuwa mgombea wa chadema aliungwa mkono na makanisa na hata uelekeo wa kampeni na hadi sasa dalili zipo wazi.Yote haya yapo kwa ajili ya maslahi ya ukristo na wala sio Uzalendo wa Utanzania kwanza.Tukumbuke mwakajana Mh.Slaa inaarifiwa alilala parokiani mjini Arusha pia matamshi ya chadema kua'tutahakikisha nchi haitawaliki' hii inamaana kuna mbinu zitatumika na nyingine zinatumika kuuchafua utawala.Hili inawezekana kwa kuwatumia watu waliomo serikalini ili kweli ionekane Kikwete hawezi na hataweza kutawala nchi hii. Matamshi ya Mwanza ya Slaa pia yalinifanya nijiulize maswali pasipo majibu 'tunataka tuikomboe nchi' sasa tunaikomboa nnchi kutoka kwa Mafisadi au kutoka utawala unaodaiwa wa Kiislam? Kweli nchi imemezwa na mdudu ufisadi na nihaki kwa kila mtu kuupiga vita kubwa,na tutambue fisadi hana dini. Kama kumpiga vita Kikwete kwa sababu ya ugumu wa maisha na ufisadi hapo sawa ila sio kwa dini yake. Udini wa Kikwete mimi siuoni na kama upo basi uleteni hapa na sote tuujue. Maandamano yanayoitishwa nchi nzima huenda yakatutumbukiza kwenye maafa ya kidini na sio kisiasa. Nasema hivi kutokana na harufua au uelekeo wa siasa za Tanzania. Tukija kwa upande wa chadema ambacho kinaungwa mkono na makanisa hili ni doa kwao chadema kwani ndani yake udini unaonekana wazi,wote tunakumbuka mwaka jana Zito Kabwe alitaka uenyekiti lakini akakataliwa mwisho wazee wakamsihi atulie naye akawasikia,nikakumbuka ile kauli ya rafiki zangu ya "muislam tena? Tumechokt",kwani ilikuwa wazi Zito angeomba urais na angepata urais misimamo ya upendeleo hakubaliani nayo hivyo angeenda haki tu! Lakini pia kumsimamisha mgombea mwenza katika nafasi ya urais mhitimu darasa la saba, haya yalikuwa matusi na dharau kwa Waislam Watanzania wote na kuwaonesha kuwa wao hawana elimu hivyo wanastahili kupewa tu nafasi za upendeleo tu.

Feb 24, 2011

MAMIA WAANDAMANA MWANZA

Kama unavyoona picha namba moja hadi namba tano hapo juu ni umati wa watu wakiwa wamehudhuria maandamano makubwa ya chadema jijini Mwanza.Picha zote zinaonesha umati ukiwa umetulia ukisikiliza kwa makini na wakati mwingine wakishangilia sana.Meya wa jiji alizomewa na mamia ya wahudhuriaji kwa madai ya kununuliwa na ccm na kuwasaliti wamachinga.Dr Slaa alipopanda jukwaani pia naye alionesha kuitikia linalosemwa na wapiga kura kua hawamtaki Mh.Josephat Manyerere ambaye ni meya wa jiji kwa kusema atamfuatilia kwa karibu zaidi kwani 'hatukukuita Dodoma na Dar es salaam bure' alisema Mh.Slaa. Naye mbunge wa Ilemela Mh.Highness Kiwia lisema ccm wamemuundia kesi kwa tuhuma za kutumia lugha za vitisho wakati wa kampeni na kununua kadi za kupigia kura. Pia Dr.Slaa amempa siku tisa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Jakaya M.Kikwete ili atoe tamko la serikali kuhusu Dowans,mfumuko wa bei na kulipuka kwa mabomu Mbagala na Gongo la Mboto la sivyo atatoa tamko. Vilevile amewataka Mawaziri wawili kujiuzuru kutokana na uzembe wao,mawaziri hao ni waziri Ngeleja na Hussein Mwinyi. Akihitimisha mkutano huo mkubwa Mh.Mbowe aliwauliza wahudhuriaji wanataka ya Misri na Tunisia? Wote wakakubali kwa sauti 'tunatakaaa'. Pia akaongeza kuwa maandamano hayo yataendelea katika mikoa yote ya kanda ya ziwa 'tunaenda kwenye wilaya zote,tukitoka hapa ni Ukerewe,tutagawana maeneo yote.Baada ya Mwanza ni Mkoa wa Mara na wilaya zake kisha Kagera,Shinyanga,Tanga,Dar es salaam,...'Mpaka kieleweke.Alisema Mh.Mbowe.Mwisho raia walitawanyika kwa amani na kurudi makwao.Baada ya kutawanyika baadhi ya wananchi walionesha hofu juu ya matamshi ya viongozi wa chadema kuwa yanahamasisha fujo. Wakitoa mfano wa kauli ni kama ile ya Dr.Slaa kuwa ni bora kuishi miaka mitano kuliko kuishi miaka mingi na ukafa kwa tiphord itakuwa aibu mbinguni. Wakati huohuo yamezuka mapigano makali kati ya Waislam na wakristo huko Mto wa Mbu mkoani Arusha.Hadi sasa ripoti zinasema makanisa kadhaa yameharibiwa.Chanzo cha vurugu inasemekana ni mkutano wa mhadhara wa wakristo uliokua unatumia Qur'an na Biblia ambapo Waislam waliona kuna kashfa,matusi na kejeli za wazi kwa Mwenyezi Mungu(ALLAH) na Mtume Muhammad(s.a.w) ndipo walijiunga na kuwavamia wakristo,hadi tunaingia mitamboni wachungaji wawili wamedhibitika kujeruhiwa na askari wakijitahidi kurudisha amani.

Feb 23, 2011

CHADEMA WAVAA MAGWANDA DARASANI.

Wanachama sugu na viongozi wa chadema tawi la Chuo kikuu cha Mt.Augustine(SAUT) Mwanza leo wametinga madarasani kuhudhuria mihadhara(lectures) wakiwa ndani ya sare(uniform) za chama chao. Wanachama hao na wapenzi wafuasi wa chadema wameonekana chuoni hapo na mavazi yao huku wanachuo wengine wakibakia kushangaa. Baada ya kufuatiliwa nyendo zao na kuhojiwa walisema hiyo ni njia moja wapo ya kuhamasisha watu kuwaunga mkono katika maandamano yatakayofanyika kesho jijini hapa.Maandamano hayo imefahamika rasmi kuwa yataanza saa saba mchana,na yakianzia Standi ya mabasi ya Buzuruga hadi viwanja vya wazi vya Furahisha maeneo ya Kiruba jijini Mwanza.Lakini baadhi ya watu wameonesha kuwa na wasiwasi wa kushiriki maandamano hayo kwa kuhofia kupigwa mabomu na risasi za moto. Pia wengine wamedai kua kesho ni siku ya kazi hivyo muda huo watakuwa wako kazini hivyo wao walipendelea ingekuwa Jumamosi au Jumapili.Mmoja wa viongozi wa tawi la chuo cha SAUT aliulizwa juu ya hofu ya mabomu alisema"tunajua wazi kuwa mabomu yatakuwepo ila sio yale ya Mbagala na Gongo la Mboto hivyo tutaandamana,lakini kwa amani".

Feb 22, 2011

GADDAFI SASA MBIONI KUNG'OKA

Rais wa muda mrefu nchini Libya Kanali Moammar Gaddafi muda si mrefu atang'oka madarakani.Hii imetokana na dunia kumshangaa kiongozi huyu kuamrisha wanajeshi kuruka na ndege za kivita dhidi ya waandamanaji na kuwarushia mabomu. Kutokana na mabomu hayo ambayo yameua watu wengi hadi sasa duru za kimataifa zimeanza kufananisha na mauaji ya kimbali.Hadi sasa watu wapatao 400 wameripotiwa kupoteza uhai,japo idadi kamili bado haijajulikana kwani pia risasi za moto zinapigwa kwa raia hao wanaoandamana kwa amani kumtaka Gaddafi kuondoka madarakani kama Mubarak na Ben Ally.Vuguvugu la maandamano kuwang'oa watawala katika nchi za kiarabu limeshika hatamu ambapo imebidi umoja wa nchi za kiarabu kuitisha kikao cha dharura ili kujaribu kuweka mambo sawa. Kutokana na hali kuwa mbaya sana nalo baraza la usalama la umoja wa mataifa limeitisha kikao ili kudhibiti mauaji yanayoendelea. Wakati huohuo mabalozi wa Libya walioko barani Asia wamejiuzulu kupinga mauaji yanayoendelea nchini Libya, na hapa sasa inaonesha mwisho wa Gaddafi umefika. Kutokana na mauajia haya ya raia wasio na hatia Gaddafi baada ya kung'olewa huenda akashtakiwa katika mahakama ya kimataifa huko nchini Uholanzi katika mahakama ya The Hague.Mwisho,tuwaombee kila dua njema ndugu zetu wa Libya waweze kufanikiwa katika lile wanalopigania na pia kuwaombea kwa Mungu wale waliouawa pia na majeruhi ili wapone haraka."MUNGU wape faraja na Amani watu wa Libya"AMIIN.

Feb 21, 2011

CHADEMA KUANDAMANA MWANZA

Chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) wamepanga kuandamana tarehe 24Februari,2011.Maandamano hayo yanayotarajiwa kua ufuasi mkubwa sikuhiyo kutokana na chama hicho kuwa na wafuasi na wapenzi wengi jijini hapa.Viongozi wa juu wa chadema wanatarajiwa kuongoza maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia stendi ya Buzuruga na kuishia kwenye uwanja wa wazi wa Furahisha uliopo Kirumba jijini hapa.Lengo kuu la maandamano hayo ni pamoja na kushinikiza Rais Kikwete ajiuzulu,kupinga mambo mbalimbali kama kupanda kwa gharama za umeme,kupinga ufisadi,kupinga Dowans kulipwa na kuongezeka kwa gharama za maisha.Kutokana na ughali wa maisha nchini maandamano hayo huenda yakasimamisha shughuli nyingi mjini na watu kwenda kuunga mkono maandamano hayo yanayotarajiwa kuanza mishale ya saa nne asubuhi.Wimbi hili la maandamano huenda likaenea mikoa yote ambayo inawafuasi wengi hasa wa upinzani.

Feb 19, 2011

MAJONZI KWA WATANZANIA.

Majonzi makubwa yametukumba tena watanzania.Mabomu yaliyolipuka Gongo la Mboto jijini Dar es salaam kwenye ghala la JWTZ la silaha limesababisha vifo na majeruhi mengi,kwani hii imetutonesha vidonda vya mabomu ya Mbagala ambayo yalisababisha maafa makubwa pia. Kidau inawafariji wahanga wote wa kadhia hiyo na kuwapa pole pamoja na dua kwa Mungu.Mungu atufanyie wepesi katika haya mazito na kutufuta machozi kutokana na majonzi haya."Eee Mungu wenye majeraha uwaponye kwa nguvu zako na waliopoteza ndugu basi wajaalie waonekane ili nyoyo zetu zifarijike".Ee Mungu tupe faraja nyoyoni mwetu na utujaalie Amani katika miji yetu, utubariki kwa mvua na mazao.Aaaamin.

Feb 16, 2011

RAIS WA CHUO CHA SAUT ANG'OLEWA.

Ndugu Patrice Jisebo Rais wa chuo cha Mt.Augustine cha jijini Mwanza ameng'olewa madarakani akiwa mwishoni mwautawala wake imefahamika.Kung'olewa kwa Rais huyo kumetokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kupokea na kuomba rushwa ili atoe huduma,pia alituhumiwa kwa ukabila katika serikali yake pamoja na utendaji usioridhisha.Tuhuma nyingine ni kuwa inasemekana alikula fedha ya ada ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na kusababisha ashindwe kufanya mitihani yake ya semester ya kwanza.Mengine ni kushindwa kusimamia masuala ya mikopo ya wanafunzi hivyo kusababisha wanafunzi wengine kuteseka kwa ukosefu wa fedha baada ya taarifa zao kucheleweshwa kwenda Bodi ya mikopo ya elimu ya juu.Pia imefahamika kua ameshindwa kusimamia ratiba ya chuo kwani mfano mitihani ya semester ya kwanza ilipaswa kuisha tarehe 30 January 2011 na masomo ya semester kuanza tarehe 1February lakini ghafla ratiba ilibadilishwa kwa baadhi ya masomo kuendelea hadi tarehe 5February ,hivyo kusababisha wengine kukosa vipindi wakati wengine wakiendelea na masomo.Aidha chanzo chetu cha kuaminika toka chuoni hapo kwa wasomi wanaotegemewa na taifa zinaendelea kubainisha kuwa ofisi ya rais huyo imekua ikivamiwa na wanafunzi kana kwamba hakuna mawaziri ili kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali hasa yale yanayohusiana na mikopo pia yeye mwenyewe rais imemlazimu kuwaondoa mawaziri katika nyadhifa zao hususan wale wa mikopo ambapo wakwanza na wapili wote waliondolewa kwa nyakati tofauti kutokana na utendaji duni.Viongozi hao walioondolewa na rais ni pamoja na Marwa aliyekua waziri wa kwanza wa mikopo akifuatiwa na Buchwa ambaye pia alisimamishwa kwa utendaji mbovu na wote wakihusishwa hasa na rushwa pamoja na majibu mabaya kwa wanachuo.Kikao cha Bunge la wanafunzi ambao walipiga kura ya kutokua na imani na rais ambapo asilimia 78 wote hawakua na imani naye kutokana na hilo madaraka ya urais alipatiwa aliyekuwa makamu wake,ambaye atakua rais hadi uchaguzi mkuu utakapoitishwa mwezi Machi hatahivyo imefahamika kuwa aliyekua rais ndugu Jisebo ambaye yuko Elimu mwaka watatu amepoteza sifa ya kutunukiwa cheti cha sifa ya urais wa SAUTSO akiwa chuoni hapo.SAUTSO ni serikali ya jumuiya ya wanachuo wa St.Augustine University.Baada ya taarifa za kung'olewa kwa rais huyo wanachuo wengi walifurahi na wachache baadhi walihuzunika kwa sababu mbalimbali.Baadhi ya wanachuo walipongeza uamuzi huo wa wabunge wao wa kikao cha tarehe 13 February ila wakasema kua kama hawakuwa na imani na rais basi serikali yote ingeng'olewa na kuwekwa ya mpito hadi uchaguzi wa mwezi machi.

Feb 15, 2011

MGOMO WA DALADALA MWANZA

Siku ya leo imekuwa ngumu kwa wakazi wa Mwanza baada ya magari ya abiria aina ya daladala kugoma kutoa huduma.Watu wenye shughuli zao katikati ya jiji wanaotoka maeneo mbalimbali walikuwa na wakati mgumu baada ya kukusa huduma hii muhimu ya usafiri.Wanafunzi ndio walikuwa na hali mbaya zaidi kwani baada ya masomo walilazimika kutembea kwa miguu,huku wengine wakiwa na njaa kali kutokana na hali ya maisha kua ngumu. Wamiliki wa magari ya daladala wamegoma ili kuishinikiza sumatra iwakubalie kupandisha nauli kutokana na bei ya mafuta kupanda. Leo magari ya watu binafsi yasiyo kwaajili ya kusafirisha abiria yalitumika kusaidia kuwapeleka na kuwarudisha abiria ndani na nje ya jiji la Mwanza kwa bei ya Tsh500 hadi 1000. Mgomo huu umeleta adha kubwa kwa watu wa kipato cha chini waishio nje kidogo ya jiji la Mwanza na vitongoji vyake, kwani iliwalazimu wengine kutembea kwa umbali mrefu ili kwenda kuusaka mkate wao wa kilasiku.Tunaiomba sumatra walitazame hili haraka ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Feb 13, 2011

YA MISRI TANZANIA HAYAWEZEKANI.

Wote tumekuwa mashahidi kwa kile kilichojitokeza nchini Misri na Tunisia kuwa wananchi wa nchi hizo wakiwa na nguvu moja na sauti moja wakiwafurusha madarakani madikteta walio kaa madarakani takribani miaka 30. Haya ni mapinduzi makubwa ya kidemokrasia kwa nchi hizo,lakini wimbi hili halitaishia Misri na Tunisia bali wimbi hili huenda likazikumba baadhi ya nchi za Kiafrika na za Kiarabu pia.Nchi kama Libya,Sudan,Zimbabwe na Uganda huenda zikaishia kwenye nguvu ya umma pia ili kuwang'oa ving'ang'anizi wa madaraka.Rais Hosni Mubarak wa Misri na Ben Ally wa Tunisia wote wameng'atuliwa na nguvu ya sauti moja ya raia wa nchi hizo.Je,hii pia inaweza kuipata Tanzania? Swali hili linahitaji kujadiliwa kwa kina,huu ndio mtazamo wangu kua haiwezekani kutokana na sababu zifuatazo; 1. Tanzania nia yetu haiko wazi kwani watu wana malengo yao na agenda zao tofauti.Hapa tofauti na agenda za udini zimejionesha wazi hivyo kuwagawa wananchi kwa misingi hiyo.Hivyo wananchi kuvunjiwa umoja wao.Wanasiasa kukana kua hakuna udini Tanzania ni sawa na kuuficha moto kwa viganja ilihali moshi unaonekana"ukificha moto moshi utakuumbua" usemi huu umedhibitika juzi baada ya viongozi wa dini kukutana pale Mövenpick na kujadili mustakbali wa amani Tanzania.Kwani wao waligundua kua udini huu utaliangamiza Taifa letu na kua kisiwa cha vurugu badala ya Amani tuliyoizoea.Kwa agenda hii kua kama Misri na Tunisia ni ngumu,kwani huenda tukaishia kuuana wenyewe kwa wenyewe. 2. Agenda ni kumng'oa Kikwete au kuing'oa CCM? Hapa mimi sielewi vema.Kama sababu ya kuhamasishana kuandamana na kugoma ni Kikwete atoke madarakani hapo pia tumeshashindwa kabla ya kuanza au kuendelea kwa nguvu,sababu ya msingi ya kumng'oa ni Uislam wake au ufisadi uliopo tangu enzi? Sote hatupendi ufisadi basi sote tusimame pamoja kuupiga vita,lakini mbona pia hapa kuna udini pia? Binafsi nimezungumza na wengi na kuhojiana nao wakidai "hatumtaki Rais muislam" ha! hili limetoka wapi?Nilishangaa na mwisho nikagundua kua kumbe tatizo sio CCM bali ni uislam wa rais. 3.Kama nia ni kuing'oa CCM na mfumo wa utawala hapo sawa! Lakini nia ya dhati ipo?mbona wapinzani hampatani? Wafuasi tumsikilize nani? Tayari huu ni mgawanyiko mwingine unao watenga raia,hivyo kuifanya dhana ya kuing'oa serikali kua ngumu. 4. Kama suala la udini litaendelea na kubezana kidini basi tumepoteza welekeo na lengo la maendeleo itakua ndozo za alinacha.Mgawanyiko huu mkubwa hauna uwezo au nguvu ya kuleta mabadiliko kwani siasa zetu sasa zimeelemewa na hisia kali na ushabiki wa hali ya juu,na bila shaka palipo na ushabiki kuna pande mbili pinzani na mwisho wa ushabiki mkali ni kuumizana. 5. Kuwepo kwa viongozi wa CCCM wanaoungwa mkono na wapinzani pia hili ni tatizo! na hii ndio inadhibitisha kua kuna agenda ya nyuma yake.Hivyo aking'oka Kikwete na wakashika madaraka wale tunao wakubali basi naona kwa agenda hii maandamano wala mapinduzi hakuna.Kwa wale wenye subira ngoja tuone 2015 kitakachotokea. Lakini kwa ubinafsi na udini hatutaweza hadi tuwe na nia na lengo moja watanzania wote. Kwa sababu hizi basi yaliyojitokeza Misri kwa Tanzania haiwezekani.Kama nia ni kuiondoa ccm nilazima wapinzani wawe wamoja na wawe na lengo moja tu. Maisha magumu sote tunaugulia, hasa sisi tulio chini mfano wamachinga,wakulima na hata wafanyakazi waaminifu na mwisho ni wale wasio na hata vimitaji pia na elimu. Kama tatizo ni UFISADI na UMASIKINI hapa Watanzania wote tutakua pamoja hadi ushindi upatikane na nafuu tuipate ila sio agenda za udini na uchama.

Feb 10, 2011

UTAJUA UMUHIMU WA KITU BAADA YA KUKIPOTEZA.

Hakika mimi nasema "huwezi kujua umuhimu na thamani ya kitu hadi kipotee".Je,tiba ni bora kuliko kinga? Ukitunza sindano mahala kisha bila kuithamini ukaweka bila kutazama ulipotunza eti kwa sababu nguo zako zote ni mpya,huna sababu ya kuitunza vema kwavile hutarajii kuitumia hiyo sindano.Nguo mpya lakini leo imetatuka na sindano hujui wapi ulipoiweka kwakuwa mwanzo haikua na thamani wala umuhimu sasa una anza kuisaka kwa kung'uta maguo na kufagia ili uipate kutokana na umuhimu wake.Baada ya kutatukiwa ndio unaona umuhimu wa sindano? Kweli umuhimu wa kitu ni hadi kipotee.Wanafunzi shuleni kila waaswalo wao hawafikiri mwisho huishia na kupata sifuri,hii ni kwa vile hawakujua thamani ya muda.Kurudia mitihani hii inaonesha mwanafunzi anatafuta alichopoteza wakati uliopita kwani wakati huo hakujua thamani na umuhimu wa masomo.Kweli thamani ya kitu huwezi kuijua mpaka kipotee.Kupotea kwa amani kunakoonekana sasa nchini tukuja kujuta na kuuguza vidonda kwani hii inaoneshwa na chokochoko zinazoendelea.Amani thamani yake kubwa,tusingoje kwenda kuitafuta mezani na p.o.p na bandeji na chongo na vilema, basi na tuone thamani yake na tuitunze. Kweli thamani ya kitu huwezi kuijua mpaka kwanza kipotee! Mfano unapesa nyingi kisha ukazifuja,vipi siku zimeisha na huna hata senti mfukoni? Thamani ya kitu huwezi kuijua mpaka kwanza kipotee. Amani kwa Watanzania ni jadi vipi leo?

Feb 8, 2011

HII NI AIBU KWA CHADEMA NA UPINZANI

Kitendo kilichofanywa na CHADEMA Bungeni mjini Dodoma ni aibu kwa chama chenyewe na upinzani kwa ujumla.Kitendo cha kukataa kanuni za bunge zisibadilishwe ili wapinzani waungane ni cha aibu na hii inaonesha CHADEMA wana agenda ya siri.Binafsi sileti ushabiki wa vyama ispokua nataka Watanzania watambue kua ubinafsi unatumaliza.Kama si ubinafsi leo tusingekua na ufisadi,nia na madhumuni kua na upinzani ni kuleta changamoto kwa serikali inayokuwa madarakani.Kugawanyika kwa wapinzani ni aibu kubwa sana ambayo haitafutika katika historia ya nchi yetu.Kukataa kwa chadema wenzao wa cuf,nccr,tlp na udp kujiunga nao katika kambi rasmi ya upinzani bungeni inaonesha chadema ni wabinafsi na hawapendi wapinzani kua na sauti moja.Je,hawa wapinzani walio nje ya kambi watakua upande gani katika suala la upinzani bungeni? Iko wazi wao wako radhi kuungana na chadema ili lao liwe moja nalo ni kua na msimamo mkali wa pamoja juu ya serikali.Kwa hoja ya cuf kuungana na ccm Zanzibar ambayo chadema kwao ndio hoja kuu, kwangu mimi hii haina mashiko.MOJA-Inaonekana kua machafuko ya Zanzibar chadema wanayapenda na amani ya Zanzibar wanaichukia,kwani lengo la cuf Zanzibar kukubali umoja nikutokana na wingi wa wafuasi wa ccm na cuf ambako imeleta mgawanyiko mkubwa na maafa hivyo ili kuwanusuru raia na roho zao ilibidi cuf kukubali kugawana madaraka.CUF Tanzania bara inajitegemea na ndio maana ina mgombea urais wake na Zanzibar mgombea wake.Hali ilivyokua Zanzibar ni hali ambayo Watanzania wote wapenda amani tuliichukia na kuombea siku moja amani ya kudumu inapatikani.Swali ni je,kwanini chadema wanakataa kuungana au kuna agenda iliyojificha.Haya tunasema hatutaki muungano na cuf kwa kuwa wao na ccm lao moja je,hawa waliobakia nao wako kwenye maridhiano na ccm? Kuna agenda gani ya siri inayowafanya kukataa kukubali madiliko ya sheria za bunge? PILI-Kauli ya Mh.Lissu haikua ya kiungwana kwani matamshi juu ya ndoa ya wake wengi na ile ya wanaume wengi ni dharau kwa watu wa Zanzibar hivyo mi naona ni vyema akaomba radhi kwa kauli hiyo.TATU-Kwa maana hii ile ndoto ya wapinzani kua na muungano wenyenguvu ili kuing'oa ccm inatoweka taratibu kwa kua na mgawanyiko mkubwa kama huu unaoonekana.NNE- Kama kanuni za bunge zilikua hazitafsiri vizuri kambi ya upinzani iweje,sasa ni wakati wa chadema kukubali ili wapinzani wawe wamoja.MWISHO-Kutoka bungeni kwenye bunge la kumi kwa chadema ni aibu.Mara ya kwanza tuliona labda ni sawa lakini kwa hili la leo la kutoka tena ili kukataa kanuni ya kuwaunga ni AIBU KUBWA.

Feb 7, 2011

VIONGOZI WA DINI KUKUTANA.

Viongozi wa dini Tanzania kukutana katika hotel ya Movenpick siku ya tarehe 9 mwezi february.Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa maandalizi Alhaji Alhad Mussa Salum ambaye ni Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam BAKWATA.Mada kuu itakua ni mustakbari wa amani Tanzania,mkutano huo utawakutanisha Masheikh,Maustadh,Maaskofu na wachungaji.Hata hivyo hakuta kuweko na waalikwa au wataalam kutoka nje ya nchi.Mada hiyo kuu ambayo ni mustakbari wa amani Tanzania na nafasi ya viongozi wa dini inatarajiwa kuleta usawa na kuridhiana baina ya wanadini baada ya kuonekana mgawanyiko wakati wa uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka jana.Mwenyekiti wa maandalizi pia aliwaomba waalikwa wote kufika ili kufanikisha mkutano huo.

Feb 6, 2011

AJALI YA MOTO

Kama unavyoona picha no.1 na no.2 hapojuu.Picha no.1 watu wakishangaa nyumba inayozimwa moto na no.2 ni gari la zimamoto maarufu kama fire.Ajali hiyo imetokea leo saa9 alasiri ambapo chanzo ilikua matairi na uchafu uliokua unachomwa kiambazani ambapo kulikua na shimo la taka.Nyumba hiyo ambayo ni Guesthouse na bar maarufu kama Kashonge iliyopo mitaa ya Nyakabungo(maarufu Genge la Mbuzi) wilani Nyamagana jijini Mwanza.Kutokana na msongamano uliopo kama moto huo ungesambaa ungesababisha hasara kubwa,hata hivyo gari la zimamoto liliwahi kufika mapema na kuonesha ni jinsi gani wanapenda na kujali kazi yao kwani leo ni jumapili.Mpaka tunaingia mitamboni ilikua bado haijajulikana hasara hasa iliyosababishwa na moto huo.

Feb 5, 2011

MH.KIKWETE HAPO UMENENA

Wakati Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa CCM nilifurahishwa na kauli yake ya kutaka Watanzania kuheshimiana katika maoni.'Msiwazomee wenye mawazo tofauti na ninyi' alisema Rais,kwani kiukweli ni kuwa hakuna kuvumiliana wakati wa kutoa maoni hususan katika mijadala ya kitaifa Rais alisema 'kutofautiana katika mawazo ni kawaida'.Tukirejea mjadala wa katiba uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah katika chuo kikuu cha Dar es salaa ambapo mtu aliyetoa maoni tofauti na mapenzi ya wengi alizomewa. Kwa wasomi kutofautiana kimawazo ni kawaida si kila hoja ya mwenzako ni sahihi au haiko sawa.Wasomi tunapojadili mambo ni sawa kutokukubaliana kutokana na vigezo vinavyokubalika na akili(logical) na pia hata sheria,hivyo kwa wasomi ukweli na halihalisi ndio hutawala nasio ushabiki na kujiwekea misimamo isiyobadilika(conservativism).Wasomi si (conservative) bali hukubaliana na hoja za kiakili (logical reasoning).Basi kwa msomi ambae hachambui vema na kuchukulia ushabiki kilajambo huyo hajaelimika na naweza kusema uwezo wake wa kuchanganua mambo ni mdogo.Mi namuunga Mkono Rais kwa kauli zake alizozitoa kwenye maadhimisho hayo ya kua 'tuvumiliane'.Basi na mimi nitumie nafasi hii kuwaomba watanzania kua kama hukubaliani na mawazo au mtazamo wa mwenzako,basi yaheshimu yale aliyoyasema na si kwa vile yuko tofauti na wewe basi azungumzalo kwako ni pumba.Msomi akizungumza pumba(pointless) lazima tumshangae basi tumpinge kwa hoja za kiakili(logica reasoning) na huo ndio usomi na kuelimika.

Feb 2, 2011

MBOWE NA CHADEMA MNATUCHANGANYA.

Mwenyekiti wa chadema taifa Mh.Freeman Mbowe jana tarehe 1/2/2011 alitoa kauli inayowachanganya wafuasi wake.Mwenyekiti huyo alitoa kauli ya kumtambua Rais ambaye mwanzo walisimama na kutangaza kutomtambua Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na hata kuungwa mkono na wapenzi na wanachama.Mh.Mbowe aliyasema hayo wakati wa kuadhimisha siku ya mahakama,ambapo Rais naye alihudhuria maazimisho hayo.Ikumbukwe kua msimamo wa kutomtambua Rais ulionekana dhahiri pale wabunge wa CHADEMA walipotoka nje wakati wa hotuba ya Rais kwa bunge."kisheria tunamtambua Rais".Swali langu ni kuwa ,pale mliposema hamumtambui rais sheria haikuwepo? Wakati wa mjadala wa bunge juu ya hotuba ya Rais,wabunge wa CHADEMA wangechangia? Sasa CHADEMA wanatuchanganya kutokana na sitaki na taka yao.Katika hotuba ya rais kuna vitu vya muhimu wabunge kujadili ambayo ni kwa maslahi ya Taifa!CHADEMA nadhani hili walilitambua na ndio maana wakaona kua wapole, je mwanzo hawakufikiri? Sasa hii inaonesha wazi kua Mh.Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma kaskazini pamoja na wabunge wengine wachache wa CHADEMA walikua sawa kukataa kutomtambua Rais na kutotoka bungeni(hawakuingia kabisa bungeni) pia inaonesha kua chama kinaongozwa na jazba na kamasivyo mbona kauli zinatoka za kujichanganya? Kwa maana hiyo CHADEMA wamelamba matapishi yao kwa kumtambua Rais ambaye mwanzo hawakumtambua.CHADEMA kueni na kauli thabiti ili kuepuka kuwaweka njiapanda wanachama na wapenzi wa chama.

Jan 30, 2011

AJALI ZA BARABARANI

Pichani gari la mizigo katikati ya jiji la Mwanza likiwa limepinduka.Gari hilo lilikua na shehena ya mkaa.Ajali hiyo imetokea kwenye kiplefti cha Mwanza hotel kwenye barabara ya Kenyatta leo alfajiri.Baada ya ajali hiyo dereva alitoweka kusikojulikana.Gari hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa magari mengine makubwa na madogo ukizingatia limeanguka katikati ya barabara.

UMEME WA BURE TUNAO.

Tanzania imekubwa na matatizo makubwa ya umeme na kusababisha mgao kila wakati.Umeme wa solar umekua sio suluhisho kwa sehemu kubwa ya Watanzania ambao ni maskini.Vifaa vya solar ni ghali hivyo kuwafanya Watanzania kuishi gizani na mapafu yao kuendelea kuathirika kutokana na moshi wa vibatari na mishumaa.Matajiri wao hawana wasiwasi kwa kuwa wanazo generator tena zenye nguvu.Serikali ya Tanzania haidhamini ugunduzi wandani,mfano kuna watu ambao wanauwezo wa kutengeneza umeme wa kutosha kwa kutumia upepo kwa gharama nafuu.Mwanajeshi mmoja mstaafu akiwa katika kipindi cha wabunifu cha ITV alionesha kipaji chake kwa kutengeneza mashine ya umeme yenye nguvu kwa kutumia hewa ya oxygen.Lakini anasema ameomba msaada serikalini hadi amechoka,hii inaonesha ni jinsi gani serikali haithamini vipaji na ugunduzi wa Watanzania.Serikali inapaswa kutoa tangazo na kuwakusanya wataalam wa aina hii na kufungua karakana ya Taifa kwa ajili ya uzalishaji wa vifaa muhimu kama mashine hii ya umeme wa oxygen.Kuzalisha mashine kama hizi kutapunguza au kuondoa kabisa utegemezi wa umeme wa maji na jua ambavyo hutegemea hali ya hewa.Mashine ya oxygen ndio suluhisho kwa matatizo ya umeme Tanzania kuliko kupotezd pesa nyingi za walipa kodi maskini kwa kununua mitambo ambayo ni ya gharama kubwa na mingine kushindwa kuzalisha.Mh.Ngeleja suluhisho ni kutumia vipaji vyetu vya ndani,tumieni pesa zetu kufanyia utafiti vifaa hivi na sio kuwalipa Richmund na DOWANS.Mitambo ikiharibika wataalam kutoka nje wanaitwa na kulipwa pesa nyingi,lakini tungekua na mitambo yetu wenyewe na wataalamu wetu wenyewe ingekua nafuu na maisha bora tunge yaona.Tumebarikiwa bahari na maziwa je,tumeshindwa kufanya utafiti juu ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji ya bahari na ziwa? Je,hatuna mainjinia? Hatuna wabunifu? Kama wapo wanatumikaje?Sio kila kitokacho magharibi na mashariki ya mbali ndio bora! Hata sisi Mungu ametubariki kua na akili si wao tu.Utaalamu wa Watanzania hautumiwi ili watu wapate wajinufaishe kwa kuingiza majenereta makontena na makontena,biashara ya mafuta nayo inoge zaidi.Wito wangu kwa serikali ni kujali na kuthamini wataalam,wagunduzi na vipaji vya Watanzania pia na kuwalinda hawa watu ambao ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa leut?

Jan 28, 2011

SABABU ZA KUCHEMSHA SHULE ZA SERIKALI.

Shule nyingi za serikali zimefanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha nne kuliko zile za misheni na za watu binafsi.Shule hizi za serikali hasa zile za kata ndizo zinazoongoza.Shule za kata zina mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa walimu hasa wenyesifa na vifaa vya kufundishia.Mbali na hayo tatitizo kubwa kabisa ni nidhamu ya walimu na wanafunzi. Walimu wengi ni vijana na wameathiriwa sana na utandawazi.Walimu wamekua wakishiriki matendo ya kingono na wanafunzi wao,pia wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wamekua washiriki wakubwa. Kutokana na hilo nidhamu kwenye shule hizi imekua ngumu sana kwani nidhamu nzuri ndio kichocheo cha taaruma nzuri. Matendo haya ngono shuleni yameleta migogoro mingi na hadi mwisho kuleta migomo,hakuna asiyejua madhara ya migomo mashuleni.Ngono kwenye shule hizi imekua kitu cha kawaida na hakuna hatua zinazochukuliwa na mamlaka hasa kwa walimu.Ukaguzi kwa kazi za walimu hakuna,na hivyo kusababisha walimu kufanya mambo yao binafsi badala ya kuhudhuria vipindi.Wakuu wa shule hizi hawakai vituoni na badala yake wamekua na mambo mengi ambayo wakati mwingine sio ya maendeleo kwa shule.Bodi za shule zimekua kama hazipo kwani kwa matatizo haya ndizo zingekua suluhisho.Kwa upande wa shule za binafsi na misheni kule sheria ni kali kwa mwanafunzi na mwalimu pia kwani makosa kama haya yatamsababishia mwalimu kufwa kazi na mwanafunzi kufukuzwa shule.Pia sera za elimu pia zinachangia sana kushindwa kwa shule hizi,mfano mtihani wa kidato chapili ulikua chekecheo na sasa baada ya kuacha wanafunzi kuendelea bila kua na uwezo ndio imesababisha masifuri mengi kidato channe.Mchujo wa kidato chapili ulikua ni muhimu sana,mfano shule za misheni kila mwaka wanafunzi huchujwa na mwisho kidato channe kubaki wenye uwezo ambapo huishia kupata daraja la kwanza na pili.Ombi langu kwa serikali ni juu ya kukariri madarasa kwa wale wanaoonekana kutokua na uwezo pia mtihani wa kidato chapili upewe hadhi yake.Sheria ziwe kali kwa walimu ili waweze kuwajibika ipasavyo na nidhamu yoa hao walimu itazamwe kwa macho mawili.Bodi za shule zipewe nguvu zaidi na wajumbe wake wawe wasomi wanaoelewa mambo ya elimu,kwani kuna baadhi ya wajumbe ni vichekesho.

WENJE AWASALITI WAMACHINGA NYAMAGANA.

Hii ni moja ya mitaa mingi ambayo ni maarufu ya Wamachinga jijini Mwanza wilayani Nyamagana.Hili ni jimbo la mbunge Mh.Wenje ambaye anaonekana kuwasaliti Wamachinga ambao ndio walio changia ushindi wake na chama chake cha CHADEMA.Mitaa mingi sasa iko tupu kutokana na amri ya Mkurugenzi wa jiji kuamuru wamachinga kwenda katika sehemu zilizopangwa kama soko la Mirongo na Mlango mmoja.Mh.Wenje anaonekana kuwasaliti kwani miongoni mwa ahadi zake ilikua ni kuhakikisha wamachinga hawabugudhiwi kama wakati wa Mh.Masha wa CCM.Katika picha hapo juu unaweza kuona ni jinsi gani ulivyo na watu wengi na mfano wake ni kama Mtaa wa Kongo na Msimbazi,hivyo mitaa hiyo ni mizuri kwa wamachinga kutokana na wingi wa watu.Watu wengi hupita maeneo haya saa za alasiri na jioni kujipatia mahitaji mbalimbali.Mtaa huu ni maarufu kwa jina la Mbananano.

Jan 25, 2011

MIUJIZA KATIKA NENO ALLAH.

Oanisha herufi hapo juu za neno Allah na mkono wako.

MIUJIZA KIGANJANI

Hakika kuna muujiza usioujua lakini leo ngoja nikufunulie.Hii si katika mambo ya kinyota ambayo wengi wanayaamini bali ni katika vidole vitano na alama zilizopo mikononi.Kwanza kabisa tazama vema picha hiyo hapo kisha tazama wakwako,vyovyote uuwekavyo uko katika umbile alilokuumbia Mola wako.Asiyeamini basi na alete hoja yake.Kuna vidole vitano kwenye mkono wako,kwa wale wajuao kiarabu kidogo itakua nafuu kwao haraka kuelewa.Kidole kidogo cha mwisho ni ALIF.Kidole cha pili na cha tatu ni LAM(double L).Cha nne yaani cha shahada ni ALIF.Na dole gumba ambalo limeshuka chini kidogo hiyo ni herufi H (he).Hivyo kiganja kutengeneza neno ALLAH kiarabu.ALIF ni sawa na A. Au ukichukua kidole kidogo ambacho ni alif (A) na vidole viwili vifuatavyo ambavyo ni double L ikifuatiwa na kidole cha shahada ni alif juu ya shada.Shada ni ile alama inayokaa juu ya double L na juu yake kuna alif. Alama hiyo kiarabu hutumika kukazia herufi mfano ni zilee double L ili kuonesha kua ni double.Kidole cha nne ni cha shahada kwa ajili ya kushuhudia kua Mungu ni mmoja. Hivyo basi kiganja kinatengeneza neno ALLAH kiarabu.Tazama maneno yaliyoandikwa ALLAH kiarabu kisha fananisha na mkono wako. Muujiza wa pili ni alama za michoro kiganjani mwako Mstari mmoja umekaa kama moja pembeni miwili japo haijaungana na mingine imeungana,mistari hiyo inatengeneza alama ya V inayotazama chini.V inayotazama chini ni nane(8) kiarabu na moja yenyewe ikosawa tu na ile unayoijua.Hivyo kila mkono uko hivyo,mkono mmoja unatengeneza namba kumi na nane(18) na mwingine themanini na moja(81). Ukijumlisha namba hizo utapata tisini na tisa(99).Mwenyezi Mungu anamajina matukufu 99. Kwa rejea isiyo rasmi Mwenyezi Mungu katika Qur'an anasema yuko karibu nasi kuliko hata mishipa yetu mikubwa ya shingo.Ndugu tafakari juu ya muujiza huu kisha jiulize kwanini wakati wa kuomba dua tunakusanya viganja pamoja?Inawezekana tunatembea na Mwenyezi Mungu kila mahali? Kwanini mwizi akatwe mkono? Kwanini Mwenyezi Mungu husema 'kwa vile ilivyovitanguliza mikono yenu'? Tafakari kisha toa maoni yako.Jamani hayo ndio niliyoyagundua katika umbile letu sisi binadamu.

Jan 23, 2011

BOMU KULIPUKA CCM

Bomu lilotegwa na kusubiri kulipuka ndani ya CCM ni lile sakata la DOWANS. Sakata hilo limeingia katika sura mpya baada ya habari za ndani ya UVCCM Mwanza zina sema fedha za malipo ya DOWANS ni fedha za uchaguzi zilizokopwa hivyo zinafanyika juhudi za kila namna ili kuzirejesha kwa njia hiyo,hilo limebainika.Blog ya KIDAU ikifanya mahojiano na mwanachama mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe mtandaoni.Mwanachama huyo aliye kwenye umoja huo wa vijana wa chama tawala aliongeza kuwa 'hii dowans ni aibu kwa chama kwani asiyejua ninani?Hatutaki dowans ilipwe kwa kua kuilipa kutasababisha chama kupoteza imani kwa wapiga kura wetu,na huo ndio msimamo wa UVCCM.Kuhusu mawaziri kukosoana hadharani alisema huo ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili,kwani wanapo mahali pa kupingana napo ni kwenye baraza la mawaziri. Akaongeza sasa kuwa bomu muda wowote litalipuka endapo wazee watailipa dowans.

WAISLAM MWANZA WAUNGA MKONO TAMKO LA DIAMOND JUBILEE

Waislam jijini Mwanza leo wakiwa wamekutana katika viwanja vya shule ya msingi Mbugani ndani ya wilaya ya Nyamagana.Kongamano hilo lilihudhuliwa na mamia ya Waislam kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikoa jirani na jiji la Mwanza.Kongamano hilo lilihutubiwa na wahadhiri maarufu ambao ni pamoja na Ustadh Ilunga Hassan kapungu pamoja na Mohammed Issa kutoka shinyanga.Mada ya kwanza ilitolewa na Ustadh Ilunga ambayo ilihusu historia ya uislam kabla ya uhuru na baada ya uhuru ambapo mada hiyo ilielezea kwa mapana madhila yaliyowakuta waislam pamoja na mfumo kristo katika serikali.Aidha mada ya pili ilielezea kuhusu katiba,ambapo Ustadh Mohammed Issa aliwataka waislam kuingia katika mjadala wa katiba badala ya kupuuzia na kusema hayo ni ya siasa.Mwisho Ustadh Kabeke alisoma tamko kwa niaba ya waislam wote na madhehebu yote. Pia suala la madai ya shule ya Msingi ya Mbugani yaliibuka tena,na hilo limetokana na uandikishwaji wa wanafunzi wapya.Shule hiyo iliyojengwa na waislam enzi za uhai wa EAMWAS na kutaifishwa na serikali ya awamu ya kwanza.Madai haya si mapya kwani shule hiyo ilikua kwenye mchakato wa kurudishwa lakini chakushangaza wanafunzi wapya wameandikishwa.Swali lilikua ni kwanini wakristo shule zao zote zimerudishwa na za waislam zimeendelea kushikiliwa na serikali.Kwapamoja Waislam waliunga mkono tamko kwa kauli moja.

Jan 22, 2011

MAGAZETI NA VYAMA VYAO

Assalaam-aleykum ndugu wanablog.Leo ninapenda kutazama mgawanyo wa magazeti kwa ajili ya habari.Kama wewe simpenzi wa chama chochote hapa nchini basi kwa habari unaweza kosa gazeti la kusoma.Kwanini basi iwehivyo? Hii imetokana na waandishi wengi kuandika habari kwa mlengo wa vyama wavipendavyo hivyo habari kujaa unazi na ushabiki.Ndugu zangu magazeti yetu yamewagawa wasomaji hivi sasa, mfano Mwanaccm hapendi magazeti ya Mwanahalisi,Rai na Tanzaniadaima na kama atanunua basi kila habari kwake anaiangalia kwa jicho la pili.Vilevile kwa upande wa Mwanachadema mambo niyaleyale hawezi kununua mfano magazeti ya Uhuru,Habarileo na Mtanzania nakama atanunua basi kila habari ataitazama kwa mtazamo hasi sawa na mwanaccm afanyavyo. Ushauri wangu kwa waandishi wa Habari ni kuwa andikeni habari zisizoegemea upande wowote ili sisi wasomaji tuwe na imani na habari zenu mnazoandika,kwani sasa tunaona habari nyingi ni za MWAMBA NGOMA.