Jan 30, 2011

AJALI ZA BARABARANI

Pichani gari la mizigo katikati ya jiji la Mwanza likiwa limepinduka.Gari hilo lilikua na shehena ya mkaa.Ajali hiyo imetokea kwenye kiplefti cha Mwanza hotel kwenye barabara ya Kenyatta leo alfajiri.Baada ya ajali hiyo dereva alitoweka kusikojulikana.Gari hilo limesababisha usumbufu mkubwa kwa magari mengine makubwa na madogo ukizingatia limeanguka katikati ya barabara.

UMEME WA BURE TUNAO.

Tanzania imekubwa na matatizo makubwa ya umeme na kusababisha mgao kila wakati.Umeme wa solar umekua sio suluhisho kwa sehemu kubwa ya Watanzania ambao ni maskini.Vifaa vya solar ni ghali hivyo kuwafanya Watanzania kuishi gizani na mapafu yao kuendelea kuathirika kutokana na moshi wa vibatari na mishumaa.Matajiri wao hawana wasiwasi kwa kuwa wanazo generator tena zenye nguvu.Serikali ya Tanzania haidhamini ugunduzi wandani,mfano kuna watu ambao wanauwezo wa kutengeneza umeme wa kutosha kwa kutumia upepo kwa gharama nafuu.Mwanajeshi mmoja mstaafu akiwa katika kipindi cha wabunifu cha ITV alionesha kipaji chake kwa kutengeneza mashine ya umeme yenye nguvu kwa kutumia hewa ya oxygen.Lakini anasema ameomba msaada serikalini hadi amechoka,hii inaonesha ni jinsi gani serikali haithamini vipaji na ugunduzi wa Watanzania.Serikali inapaswa kutoa tangazo na kuwakusanya wataalam wa aina hii na kufungua karakana ya Taifa kwa ajili ya uzalishaji wa vifaa muhimu kama mashine hii ya umeme wa oxygen.Kuzalisha mashine kama hizi kutapunguza au kuondoa kabisa utegemezi wa umeme wa maji na jua ambavyo hutegemea hali ya hewa.Mashine ya oxygen ndio suluhisho kwa matatizo ya umeme Tanzania kuliko kupotezd pesa nyingi za walipa kodi maskini kwa kununua mitambo ambayo ni ya gharama kubwa na mingine kushindwa kuzalisha.Mh.Ngeleja suluhisho ni kutumia vipaji vyetu vya ndani,tumieni pesa zetu kufanyia utafiti vifaa hivi na sio kuwalipa Richmund na DOWANS.Mitambo ikiharibika wataalam kutoka nje wanaitwa na kulipwa pesa nyingi,lakini tungekua na mitambo yetu wenyewe na wataalamu wetu wenyewe ingekua nafuu na maisha bora tunge yaona.Tumebarikiwa bahari na maziwa je,tumeshindwa kufanya utafiti juu ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji ya bahari na ziwa? Je,hatuna mainjinia? Hatuna wabunifu? Kama wapo wanatumikaje?Sio kila kitokacho magharibi na mashariki ya mbali ndio bora! Hata sisi Mungu ametubariki kua na akili si wao tu.Utaalamu wa Watanzania hautumiwi ili watu wapate wajinufaishe kwa kuingiza majenereta makontena na makontena,biashara ya mafuta nayo inoge zaidi.Wito wangu kwa serikali ni kujali na kuthamini wataalam,wagunduzi na vipaji vya Watanzania pia na kuwalinda hawa watu ambao ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa leut?

Jan 28, 2011

SABABU ZA KUCHEMSHA SHULE ZA SERIKALI.

Shule nyingi za serikali zimefanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha nne kuliko zile za misheni na za watu binafsi.Shule hizi za serikali hasa zile za kata ndizo zinazoongoza.Shule za kata zina mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa walimu hasa wenyesifa na vifaa vya kufundishia.Mbali na hayo tatitizo kubwa kabisa ni nidhamu ya walimu na wanafunzi. Walimu wengi ni vijana na wameathiriwa sana na utandawazi.Walimu wamekua wakishiriki matendo ya kingono na wanafunzi wao,pia wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wamekua washiriki wakubwa. Kutokana na hilo nidhamu kwenye shule hizi imekua ngumu sana kwani nidhamu nzuri ndio kichocheo cha taaruma nzuri. Matendo haya ngono shuleni yameleta migogoro mingi na hadi mwisho kuleta migomo,hakuna asiyejua madhara ya migomo mashuleni.Ngono kwenye shule hizi imekua kitu cha kawaida na hakuna hatua zinazochukuliwa na mamlaka hasa kwa walimu.Ukaguzi kwa kazi za walimu hakuna,na hivyo kusababisha walimu kufanya mambo yao binafsi badala ya kuhudhuria vipindi.Wakuu wa shule hizi hawakai vituoni na badala yake wamekua na mambo mengi ambayo wakati mwingine sio ya maendeleo kwa shule.Bodi za shule zimekua kama hazipo kwani kwa matatizo haya ndizo zingekua suluhisho.Kwa upande wa shule za binafsi na misheni kule sheria ni kali kwa mwanafunzi na mwalimu pia kwani makosa kama haya yatamsababishia mwalimu kufwa kazi na mwanafunzi kufukuzwa shule.Pia sera za elimu pia zinachangia sana kushindwa kwa shule hizi,mfano mtihani wa kidato chapili ulikua chekecheo na sasa baada ya kuacha wanafunzi kuendelea bila kua na uwezo ndio imesababisha masifuri mengi kidato channe.Mchujo wa kidato chapili ulikua ni muhimu sana,mfano shule za misheni kila mwaka wanafunzi huchujwa na mwisho kidato channe kubaki wenye uwezo ambapo huishia kupata daraja la kwanza na pili.Ombi langu kwa serikali ni juu ya kukariri madarasa kwa wale wanaoonekana kutokua na uwezo pia mtihani wa kidato chapili upewe hadhi yake.Sheria ziwe kali kwa walimu ili waweze kuwajibika ipasavyo na nidhamu yoa hao walimu itazamwe kwa macho mawili.Bodi za shule zipewe nguvu zaidi na wajumbe wake wawe wasomi wanaoelewa mambo ya elimu,kwani kuna baadhi ya wajumbe ni vichekesho.

WENJE AWASALITI WAMACHINGA NYAMAGANA.

Hii ni moja ya mitaa mingi ambayo ni maarufu ya Wamachinga jijini Mwanza wilayani Nyamagana.Hili ni jimbo la mbunge Mh.Wenje ambaye anaonekana kuwasaliti Wamachinga ambao ndio walio changia ushindi wake na chama chake cha CHADEMA.Mitaa mingi sasa iko tupu kutokana na amri ya Mkurugenzi wa jiji kuamuru wamachinga kwenda katika sehemu zilizopangwa kama soko la Mirongo na Mlango mmoja.Mh.Wenje anaonekana kuwasaliti kwani miongoni mwa ahadi zake ilikua ni kuhakikisha wamachinga hawabugudhiwi kama wakati wa Mh.Masha wa CCM.Katika picha hapo juu unaweza kuona ni jinsi gani ulivyo na watu wengi na mfano wake ni kama Mtaa wa Kongo na Msimbazi,hivyo mitaa hiyo ni mizuri kwa wamachinga kutokana na wingi wa watu.Watu wengi hupita maeneo haya saa za alasiri na jioni kujipatia mahitaji mbalimbali.Mtaa huu ni maarufu kwa jina la Mbananano.

Jan 25, 2011

MIUJIZA KATIKA NENO ALLAH.

Oanisha herufi hapo juu za neno Allah na mkono wako.

MIUJIZA KIGANJANI

Hakika kuna muujiza usioujua lakini leo ngoja nikufunulie.Hii si katika mambo ya kinyota ambayo wengi wanayaamini bali ni katika vidole vitano na alama zilizopo mikononi.Kwanza kabisa tazama vema picha hiyo hapo kisha tazama wakwako,vyovyote uuwekavyo uko katika umbile alilokuumbia Mola wako.Asiyeamini basi na alete hoja yake.Kuna vidole vitano kwenye mkono wako,kwa wale wajuao kiarabu kidogo itakua nafuu kwao haraka kuelewa.Kidole kidogo cha mwisho ni ALIF.Kidole cha pili na cha tatu ni LAM(double L).Cha nne yaani cha shahada ni ALIF.Na dole gumba ambalo limeshuka chini kidogo hiyo ni herufi H (he).Hivyo kiganja kutengeneza neno ALLAH kiarabu.ALIF ni sawa na A. Au ukichukua kidole kidogo ambacho ni alif (A) na vidole viwili vifuatavyo ambavyo ni double L ikifuatiwa na kidole cha shahada ni alif juu ya shada.Shada ni ile alama inayokaa juu ya double L na juu yake kuna alif. Alama hiyo kiarabu hutumika kukazia herufi mfano ni zilee double L ili kuonesha kua ni double.Kidole cha nne ni cha shahada kwa ajili ya kushuhudia kua Mungu ni mmoja. Hivyo basi kiganja kinatengeneza neno ALLAH kiarabu.Tazama maneno yaliyoandikwa ALLAH kiarabu kisha fananisha na mkono wako. Muujiza wa pili ni alama za michoro kiganjani mwako Mstari mmoja umekaa kama moja pembeni miwili japo haijaungana na mingine imeungana,mistari hiyo inatengeneza alama ya V inayotazama chini.V inayotazama chini ni nane(8) kiarabu na moja yenyewe ikosawa tu na ile unayoijua.Hivyo kila mkono uko hivyo,mkono mmoja unatengeneza namba kumi na nane(18) na mwingine themanini na moja(81). Ukijumlisha namba hizo utapata tisini na tisa(99).Mwenyezi Mungu anamajina matukufu 99. Kwa rejea isiyo rasmi Mwenyezi Mungu katika Qur'an anasema yuko karibu nasi kuliko hata mishipa yetu mikubwa ya shingo.Ndugu tafakari juu ya muujiza huu kisha jiulize kwanini wakati wa kuomba dua tunakusanya viganja pamoja?Inawezekana tunatembea na Mwenyezi Mungu kila mahali? Kwanini mwizi akatwe mkono? Kwanini Mwenyezi Mungu husema 'kwa vile ilivyovitanguliza mikono yenu'? Tafakari kisha toa maoni yako.Jamani hayo ndio niliyoyagundua katika umbile letu sisi binadamu.

Jan 23, 2011

BOMU KULIPUKA CCM

Bomu lilotegwa na kusubiri kulipuka ndani ya CCM ni lile sakata la DOWANS. Sakata hilo limeingia katika sura mpya baada ya habari za ndani ya UVCCM Mwanza zina sema fedha za malipo ya DOWANS ni fedha za uchaguzi zilizokopwa hivyo zinafanyika juhudi za kila namna ili kuzirejesha kwa njia hiyo,hilo limebainika.Blog ya KIDAU ikifanya mahojiano na mwanachama mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe mtandaoni.Mwanachama huyo aliye kwenye umoja huo wa vijana wa chama tawala aliongeza kuwa 'hii dowans ni aibu kwa chama kwani asiyejua ninani?Hatutaki dowans ilipwe kwa kua kuilipa kutasababisha chama kupoteza imani kwa wapiga kura wetu,na huo ndio msimamo wa UVCCM.Kuhusu mawaziri kukosoana hadharani alisema huo ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili,kwani wanapo mahali pa kupingana napo ni kwenye baraza la mawaziri. Akaongeza sasa kuwa bomu muda wowote litalipuka endapo wazee watailipa dowans.

WAISLAM MWANZA WAUNGA MKONO TAMKO LA DIAMOND JUBILEE

Waislam jijini Mwanza leo wakiwa wamekutana katika viwanja vya shule ya msingi Mbugani ndani ya wilaya ya Nyamagana.Kongamano hilo lilihudhuliwa na mamia ya Waislam kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikoa jirani na jiji la Mwanza.Kongamano hilo lilihutubiwa na wahadhiri maarufu ambao ni pamoja na Ustadh Ilunga Hassan kapungu pamoja na Mohammed Issa kutoka shinyanga.Mada ya kwanza ilitolewa na Ustadh Ilunga ambayo ilihusu historia ya uislam kabla ya uhuru na baada ya uhuru ambapo mada hiyo ilielezea kwa mapana madhila yaliyowakuta waislam pamoja na mfumo kristo katika serikali.Aidha mada ya pili ilielezea kuhusu katiba,ambapo Ustadh Mohammed Issa aliwataka waislam kuingia katika mjadala wa katiba badala ya kupuuzia na kusema hayo ni ya siasa.Mwisho Ustadh Kabeke alisoma tamko kwa niaba ya waislam wote na madhehebu yote. Pia suala la madai ya shule ya Msingi ya Mbugani yaliibuka tena,na hilo limetokana na uandikishwaji wa wanafunzi wapya.Shule hiyo iliyojengwa na waislam enzi za uhai wa EAMWAS na kutaifishwa na serikali ya awamu ya kwanza.Madai haya si mapya kwani shule hiyo ilikua kwenye mchakato wa kurudishwa lakini chakushangaza wanafunzi wapya wameandikishwa.Swali lilikua ni kwanini wakristo shule zao zote zimerudishwa na za waislam zimeendelea kushikiliwa na serikali.Kwapamoja Waislam waliunga mkono tamko kwa kauli moja.

Jan 22, 2011

MAGAZETI NA VYAMA VYAO

Assalaam-aleykum ndugu wanablog.Leo ninapenda kutazama mgawanyo wa magazeti kwa ajili ya habari.Kama wewe simpenzi wa chama chochote hapa nchini basi kwa habari unaweza kosa gazeti la kusoma.Kwanini basi iwehivyo? Hii imetokana na waandishi wengi kuandika habari kwa mlengo wa vyama wavipendavyo hivyo habari kujaa unazi na ushabiki.Ndugu zangu magazeti yetu yamewagawa wasomaji hivi sasa, mfano Mwanaccm hapendi magazeti ya Mwanahalisi,Rai na Tanzaniadaima na kama atanunua basi kila habari kwake anaiangalia kwa jicho la pili.Vilevile kwa upande wa Mwanachadema mambo niyaleyale hawezi kununua mfano magazeti ya Uhuru,Habarileo na Mtanzania nakama atanunua basi kila habari ataitazama kwa mtazamo hasi sawa na mwanaccm afanyavyo. Ushauri wangu kwa waandishi wa Habari ni kuwa andikeni habari zisizoegemea upande wowote ili sisi wasomaji tuwe na imani na habari zenu mnazoandika,kwani sasa tunaona habari nyingi ni za MWAMBA NGOMA.