Jan 25, 2011

MIUJIZA KIGANJANI

Hakika kuna muujiza usioujua lakini leo ngoja nikufunulie.Hii si katika mambo ya kinyota ambayo wengi wanayaamini bali ni katika vidole vitano na alama zilizopo mikononi.Kwanza kabisa tazama vema picha hiyo hapo kisha tazama wakwako,vyovyote uuwekavyo uko katika umbile alilokuumbia Mola wako.Asiyeamini basi na alete hoja yake.Kuna vidole vitano kwenye mkono wako,kwa wale wajuao kiarabu kidogo itakua nafuu kwao haraka kuelewa.Kidole kidogo cha mwisho ni ALIF.Kidole cha pili na cha tatu ni LAM(double L).Cha nne yaani cha shahada ni ALIF.Na dole gumba ambalo limeshuka chini kidogo hiyo ni herufi H (he).Hivyo kiganja kutengeneza neno ALLAH kiarabu.ALIF ni sawa na A. Au ukichukua kidole kidogo ambacho ni alif (A) na vidole viwili vifuatavyo ambavyo ni double L ikifuatiwa na kidole cha shahada ni alif juu ya shada.Shada ni ile alama inayokaa juu ya double L na juu yake kuna alif. Alama hiyo kiarabu hutumika kukazia herufi mfano ni zilee double L ili kuonesha kua ni double.Kidole cha nne ni cha shahada kwa ajili ya kushuhudia kua Mungu ni mmoja. Hivyo basi kiganja kinatengeneza neno ALLAH kiarabu.Tazama maneno yaliyoandikwa ALLAH kiarabu kisha fananisha na mkono wako. Muujiza wa pili ni alama za michoro kiganjani mwako Mstari mmoja umekaa kama moja pembeni miwili japo haijaungana na mingine imeungana,mistari hiyo inatengeneza alama ya V inayotazama chini.V inayotazama chini ni nane(8) kiarabu na moja yenyewe ikosawa tu na ile unayoijua.Hivyo kila mkono uko hivyo,mkono mmoja unatengeneza namba kumi na nane(18) na mwingine themanini na moja(81). Ukijumlisha namba hizo utapata tisini na tisa(99).Mwenyezi Mungu anamajina matukufu 99. Kwa rejea isiyo rasmi Mwenyezi Mungu katika Qur'an anasema yuko karibu nasi kuliko hata mishipa yetu mikubwa ya shingo.Ndugu tafakari juu ya muujiza huu kisha jiulize kwanini wakati wa kuomba dua tunakusanya viganja pamoja?Inawezekana tunatembea na Mwenyezi Mungu kila mahali? Kwanini mwizi akatwe mkono? Kwanini Mwenyezi Mungu husema 'kwa vile ilivyovitanguliza mikono yenu'? Tafakari kisha toa maoni yako.Jamani hayo ndio niliyoyagundua katika umbile letu sisi binadamu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.