Jan 28, 2011

SABABU ZA KUCHEMSHA SHULE ZA SERIKALI.

Shule nyingi za serikali zimefanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha nne kuliko zile za misheni na za watu binafsi.Shule hizi za serikali hasa zile za kata ndizo zinazoongoza.Shule za kata zina mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa walimu hasa wenyesifa na vifaa vya kufundishia.Mbali na hayo tatitizo kubwa kabisa ni nidhamu ya walimu na wanafunzi. Walimu wengi ni vijana na wameathiriwa sana na utandawazi.Walimu wamekua wakishiriki matendo ya kingono na wanafunzi wao,pia wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wamekua washiriki wakubwa. Kutokana na hilo nidhamu kwenye shule hizi imekua ngumu sana kwani nidhamu nzuri ndio kichocheo cha taaruma nzuri. Matendo haya ngono shuleni yameleta migogoro mingi na hadi mwisho kuleta migomo,hakuna asiyejua madhara ya migomo mashuleni.Ngono kwenye shule hizi imekua kitu cha kawaida na hakuna hatua zinazochukuliwa na mamlaka hasa kwa walimu.Ukaguzi kwa kazi za walimu hakuna,na hivyo kusababisha walimu kufanya mambo yao binafsi badala ya kuhudhuria vipindi.Wakuu wa shule hizi hawakai vituoni na badala yake wamekua na mambo mengi ambayo wakati mwingine sio ya maendeleo kwa shule.Bodi za shule zimekua kama hazipo kwani kwa matatizo haya ndizo zingekua suluhisho.Kwa upande wa shule za binafsi na misheni kule sheria ni kali kwa mwanafunzi na mwalimu pia kwani makosa kama haya yatamsababishia mwalimu kufwa kazi na mwanafunzi kufukuzwa shule.Pia sera za elimu pia zinachangia sana kushindwa kwa shule hizi,mfano mtihani wa kidato chapili ulikua chekecheo na sasa baada ya kuacha wanafunzi kuendelea bila kua na uwezo ndio imesababisha masifuri mengi kidato channe.Mchujo wa kidato chapili ulikua ni muhimu sana,mfano shule za misheni kila mwaka wanafunzi huchujwa na mwisho kidato channe kubaki wenye uwezo ambapo huishia kupata daraja la kwanza na pili.Ombi langu kwa serikali ni juu ya kukariri madarasa kwa wale wanaoonekana kutokua na uwezo pia mtihani wa kidato chapili upewe hadhi yake.Sheria ziwe kali kwa walimu ili waweze kuwajibika ipasavyo na nidhamu yoa hao walimu itazamwe kwa macho mawili.Bodi za shule zipewe nguvu zaidi na wajumbe wake wawe wasomi wanaoelewa mambo ya elimu,kwani kuna baadhi ya wajumbe ni vichekesho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.