Jan 30, 2011

UMEME WA BURE TUNAO.

Tanzania imekubwa na matatizo makubwa ya umeme na kusababisha mgao kila wakati.Umeme wa solar umekua sio suluhisho kwa sehemu kubwa ya Watanzania ambao ni maskini.Vifaa vya solar ni ghali hivyo kuwafanya Watanzania kuishi gizani na mapafu yao kuendelea kuathirika kutokana na moshi wa vibatari na mishumaa.Matajiri wao hawana wasiwasi kwa kuwa wanazo generator tena zenye nguvu.Serikali ya Tanzania haidhamini ugunduzi wandani,mfano kuna watu ambao wanauwezo wa kutengeneza umeme wa kutosha kwa kutumia upepo kwa gharama nafuu.Mwanajeshi mmoja mstaafu akiwa katika kipindi cha wabunifu cha ITV alionesha kipaji chake kwa kutengeneza mashine ya umeme yenye nguvu kwa kutumia hewa ya oxygen.Lakini anasema ameomba msaada serikalini hadi amechoka,hii inaonesha ni jinsi gani serikali haithamini vipaji na ugunduzi wa Watanzania.Serikali inapaswa kutoa tangazo na kuwakusanya wataalam wa aina hii na kufungua karakana ya Taifa kwa ajili ya uzalishaji wa vifaa muhimu kama mashine hii ya umeme wa oxygen.Kuzalisha mashine kama hizi kutapunguza au kuondoa kabisa utegemezi wa umeme wa maji na jua ambavyo hutegemea hali ya hewa.Mashine ya oxygen ndio suluhisho kwa matatizo ya umeme Tanzania kuliko kupotezd pesa nyingi za walipa kodi maskini kwa kununua mitambo ambayo ni ya gharama kubwa na mingine kushindwa kuzalisha.Mh.Ngeleja suluhisho ni kutumia vipaji vyetu vya ndani,tumieni pesa zetu kufanyia utafiti vifaa hivi na sio kuwalipa Richmund na DOWANS.Mitambo ikiharibika wataalam kutoka nje wanaitwa na kulipwa pesa nyingi,lakini tungekua na mitambo yetu wenyewe na wataalamu wetu wenyewe ingekua nafuu na maisha bora tunge yaona.Tumebarikiwa bahari na maziwa je,tumeshindwa kufanya utafiti juu ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji ya bahari na ziwa? Je,hatuna mainjinia? Hatuna wabunifu? Kama wapo wanatumikaje?Sio kila kitokacho magharibi na mashariki ya mbali ndio bora! Hata sisi Mungu ametubariki kua na akili si wao tu.Utaalamu wa Watanzania hautumiwi ili watu wapate wajinufaishe kwa kuingiza majenereta makontena na makontena,biashara ya mafuta nayo inoge zaidi.Wito wangu kwa serikali ni kujali na kuthamini wataalam,wagunduzi na vipaji vya Watanzania pia na kuwalinda hawa watu ambao ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa leut?

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.