Jan 23, 2011

WAISLAM MWANZA WAUNGA MKONO TAMKO LA DIAMOND JUBILEE

Waislam jijini Mwanza leo wakiwa wamekutana katika viwanja vya shule ya msingi Mbugani ndani ya wilaya ya Nyamagana.Kongamano hilo lilihudhuliwa na mamia ya Waislam kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikoa jirani na jiji la Mwanza.Kongamano hilo lilihutubiwa na wahadhiri maarufu ambao ni pamoja na Ustadh Ilunga Hassan kapungu pamoja na Mohammed Issa kutoka shinyanga.Mada ya kwanza ilitolewa na Ustadh Ilunga ambayo ilihusu historia ya uislam kabla ya uhuru na baada ya uhuru ambapo mada hiyo ilielezea kwa mapana madhila yaliyowakuta waislam pamoja na mfumo kristo katika serikali.Aidha mada ya pili ilielezea kuhusu katiba,ambapo Ustadh Mohammed Issa aliwataka waislam kuingia katika mjadala wa katiba badala ya kupuuzia na kusema hayo ni ya siasa.Mwisho Ustadh Kabeke alisoma tamko kwa niaba ya waislam wote na madhehebu yote. Pia suala la madai ya shule ya Msingi ya Mbugani yaliibuka tena,na hilo limetokana na uandikishwaji wa wanafunzi wapya.Shule hiyo iliyojengwa na waislam enzi za uhai wa EAMWAS na kutaifishwa na serikali ya awamu ya kwanza.Madai haya si mapya kwani shule hiyo ilikua kwenye mchakato wa kurudishwa lakini chakushangaza wanafunzi wapya wameandikishwa.Swali lilikua ni kwanini wakristo shule zao zote zimerudishwa na za waislam zimeendelea kushikiliwa na serikali.Kwapamoja Waislam waliunga mkono tamko kwa kauli moja.

1 comment:

  1. Salaam. Mwezi mmoja waliotoa waislam kurejeshewa shule ya Mbugani umepita? vipi wamepewa? wamechukua hatua gani? au ulikuwa mkwara wa nyau tu?

    ReplyDelete

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.