Jan 28, 2011

WENJE AWASALITI WAMACHINGA NYAMAGANA.

Hii ni moja ya mitaa mingi ambayo ni maarufu ya Wamachinga jijini Mwanza wilayani Nyamagana.Hili ni jimbo la mbunge Mh.Wenje ambaye anaonekana kuwasaliti Wamachinga ambao ndio walio changia ushindi wake na chama chake cha CHADEMA.Mitaa mingi sasa iko tupu kutokana na amri ya Mkurugenzi wa jiji kuamuru wamachinga kwenda katika sehemu zilizopangwa kama soko la Mirongo na Mlango mmoja.Mh.Wenje anaonekana kuwasaliti kwani miongoni mwa ahadi zake ilikua ni kuhakikisha wamachinga hawabugudhiwi kama wakati wa Mh.Masha wa CCM.Katika picha hapo juu unaweza kuona ni jinsi gani ulivyo na watu wengi na mfano wake ni kama Mtaa wa Kongo na Msimbazi,hivyo mitaa hiyo ni mizuri kwa wamachinga kutokana na wingi wa watu.Watu wengi hupita maeneo haya saa za alasiri na jioni kujipatia mahitaji mbalimbali.Mtaa huu ni maarufu kwa jina la Mbananano.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.