Mar 26, 2011

WIMBO HUU TBCtaifa HAPANA.

Wimbo wimbo unaotumiwa kama kidokezo cha hotuba za hayati Mwl.Nyeree TBCtaifa kwakweli ni upotoshaji mkubwa wa historia ya Tanganyika.Muda mrefu wimbo huu nimekuwa nikiutathmini na kuutafakari na kukosa majibu kwa siku nyingi lakini sasa hatimaye nimegundua kisa na mkasa wa haya yote. Wimbo unasema "...kama sio juhudi zako Nyerere na uhuru tungepata wapi...? Kama sio juhudi zako Nyerere na amani tungepata wapi...?" Hii ni sehemu ya wimbo huo na mashairi yake ndio yaliyosababisha leo niseme haya nitakayosema.1.Watunzi wa wimbo huu na walioleta wazo la wimbo na wapigaji wa wimbo wanalengo la kuipoteza historia yote ya wapigania uhuru na kuonesha kuwa juhudi zote na kazi yote ya uhuru kafanya nyerere pekee. 2.Lengo ni kuonesha kuwa Nyerere ndio mwasisi wa mwanzo na wa mwisho wa harakati za kupigania uhuru na kuonesha au kukiaminisha kizazi kipya na kijacho kuwa Nyerere ndiye shujaa pekee katika historia ya Tanganyika.3. Wale wote waliojitolea kwa mali zao pia kumpa dhamana Nyerere kuwa kiongozi katika chama ambacho hakukianzisha na ambacho kilikuwa na malengo wala hawatajwi wala kupewa sifa na kuthaminiwa kuwa ni watu muhimu katika historia ya nchi yetu.Vitabu vya historia pia vyafuata mkumbo huohuo wa kumsifu Nyerere.4.Wimbo huu unaopigwa TBCtaifa usimamishwe maramoja na kutafutwa wimbo au kutafutwa kidokezo mbadala ambacho kinawatambua au kutambua juhudi za waasisi wa harakati za uhuru.Kupindishwa kwa historia ya Tanganyika ni juhudi za makusudi za kundi fulani kutaka kuonesha kuwa kundi jingine halina mchango wala halikuwa na mchango wowote katika mbio za kusaka uhuru.Kumbuka kuwa wakati wengine wakihudhuria ibada pamoja na wakoloni kundi la pili lilihangaika kuusaka uhuru wa nchi hii. Kundi hilo lililokula sahani moja na wakoloni leo linaeneza chuki za kidini kwa kueneza nyaraka za siri kwenye nyumba za ibada.Wakati kundi moja likidharauliwa kundi jingine linajineemesha na mikataba mbalimbali pia kupata misaada. Naomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya watu wachache wenye tabia hii mbaya ambayo muda si mrefu italiangamiza taifa.Serikali iandae majina halisi ya wapambanaji wa harakati za uhuru wote pasipo kumbagua yeyote miongoni mwao.Historia sahihi ya Tanganyika iandikwe kwani kuna uongo mwingi unaowekwa au uliowekwa kwenye historia na mfano mdogo ni kama wimbo huu wa wosia wa mwl.Nyerere kwenye redio ya Taifa. Kizazi kijacho hakitaijua historia na mashujaa kwa kuwa hawatajwi hata maramoja na hata serikali nayo iko kimya. Kweli wimbo huu ni mwiba kwa historia na kizazi kipya hakitawajua mashujaa bali Nyerere pekee.

Mar 21, 2011

DR.KIKWETE JIBU HOJA YA DR.SLAA.

Dr.Slaa mara kwa mara amekuwa akimtaja Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete katika kashfa za ufisadi. Katika ile the list of shame Rais kikwete alitajwa,na kutajwa huku kunatajwa hadharani kweupe lakini Rais Kikwete alijibu tu kuwa yeye si mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans. Rais Kikwete amehusishwa pia na Kagoda ambayo imevuna mabilioni ya mipesa katika akauti ya madeni ya nje ya EPA. Dr.Slaa amekuwa na kiburi cha kusema na kutaja kwa ujasiri mkubwa sana majukwaani, lakini hadi sasa hajafikishwa mahakamani kama alivyoburuzwa Mchungaji Christopher Mtikila alipo mdhihaki Rais. Hoja kuu iliyopo hapa ili kuondoa wasiwasi kwetu sisi raia tunataka Dr.Wilbrod Slaa afikishwe mahakamani kwa kumhusisha Rais na ufisadi.Kushindwa kumpeleka au kumshtaki Dr.Slaa inamaanisha ni kweli Dr.Slaa anao ushahidi wa wazi juu ya vitendo vya ufisadi kwa Rais Kikwete. Sasa hamu na shauku yetu wananchi ni kuona mahakama inatikisika kwa Dr.Slaa kufikishwa mahakamani. Ukimya wa mamlaka ya nchi kukaa kimya inatupa wasiwasi sana na kuamini kuwa yote yasemwayo ni kweli.Mwisho,nasisitiza tena na tena Dr.Slaa afikishwe mahakamani, na hoja zake pia zijibiwe kuliko kukaa kimya.

Mar 18, 2011

ASKOFU RWUA'ICHI UMETUDANGANYA.

Askofu wa jimbo la Mwanza ndugu Rwua'ichi jana alikana kanisa Katoliki kukiunga mkono chama cha CHADEMA wakati akihojiwa na shirika la utangazaji Tanzania TBC1. Askofu alisema kuwa wakatoliki wako katika kila chama,hivyo yeye anashangazwa na habari hizo za kanisa lake kukiunga mkono CHADEMA. Hakika siasa zinazoendelea katika nchi yetu ni mbaya sana na hatua makusudi zisipochukuliwa basi umoja na amani ya Tanzania itatoweka na kuirejesha itakuwa tabu.Nataka kumuonesha Askofu jinsi ambavyo hakusema kweli, na sio rahisi kwa yeyote hata Kardinali Pengo hawezi kulikili hili hata siku moja.Mara nyingi hutokea na kukanwa mambo yanapobainika mfano kuna vitabu vilikuwa sokoni vikaondolewa baada ya kubainika vina mikakati ya siri ambayo mingine imetekelezwa na mingine ikitarajiwa. Askofu ametudanganya wapi? Hebu na akumbuke waraka wa Kardinali Pengo wa miaka ya 90 ambao tunaamini ndio ulio sababisha mauaji ya Mwembechai.Kwani kwenye waraka huo Pengo analalamikia mihadhara na umoja wa waislam kuwa ni hatari kwa Ukristo Tanzania na baadae likaibuka kundi la Wakristo waliosomeshwa Qur'an na matokeo yake au adhali zake ni kama zile za Mto wa Mbu kule Arusha, japo haitajaripotiwa lakini hata Mwanza ugomvi uliwahi kutokea mwaka 2010 miezi ya mwanzo pale kwenye viwanja vya mbugani palipokuwa panafanyika mdahalo kati ya waislam na wakristo na baadhi kuumia kidogo.Askofu Rwua'chi ni wazi hawezi kusema hadharani juu ya kukiunga mkono chama cha chadema, kwani wakati wa uchaguzi zilitolewa nyaraka kwa makanisa yote ili wakristo wote wachague chadema.Waraka huo wa mwisho kabla ya uchaguzi ulitoa tahadhali kwa wakristo hasa viongozi kuwa waraka huo ni kwaajili ya viongozi tu na muumini wa kawaida haruhusiwi kuuona ispokuwa kazi kubwa itakuwa kufikisha ujumbe kwa njia ya mahubiri. CCM na CUF ni vyama vya waislam hivyo tukichague chama chetu cha chadema ilisema sehemu ya waraka huo kwa makanisa.Uungaji mkono wa kanisa ni kwa chadema umedhihilika Mkoni Rukwa ambako waumini walioonekana kukiunga mkono chama cha CCM walifukuzwa ushirika. Rukwa ni mbali nami, lakini chuki kwa wakristo chuki kubwa imepandikizwa juu ya waislam na viongozi wenye majina ya kiislam.Haya nayajua kutokana nakuwa naishi na wakristo na mengi huzungumzwa, asilimia tisini ya watu nifanyao nao kazi muda wote ni wakristo na inapoibuka mijadala ya wazi wao pia hujipambanua na hata kusema waliyoelekezwa kutenda. Kwahaya mimi naamini askofu hakusema kweli kwani halihalisi inajionesha wazi.Kuna wale wanaoamini kua magazeti hayasomwi na wengi lakini ukweli wa magazeti sikuhizi umebadilika kwani watunasoma magazeti mtandaoni na mengine kuchambuliwa redioni, na baadhi ya magazeti yana chochea uvunjifu wa amani na kuligawa taifa, hasa kwa kuwaaminisha wasomaji kuwa Viongozi wote wakuu ambao ni waislam hawanatija kwa Taifa na hawajui uongozi.Mpaka sasa nchi imegawanyika, rejea makala yangu ya nyuma isemayo "ya misri hayawezekani tanzania".Kanisa linao wajibu wa kuhubiri amani na upendo makanisani kwani chuki juu ya waislam iko wazi,asiamini na ajaribu kuingia Jamiiforums.com na aone vile post zinazohusu waislam au uislam zilivyo chafu au akae na kikundi chochote cha wakristo na asikilize mada juu ya waislam na uislam,utaona jinsi chuki ilivyo. Utagundua kuwa hakuna mkristo yoyote ambaye anashirikiana na wakristo hata kama ni kwa kiwango cha chini ni shabiki mfuasi mkubwa wa chadema,hii pia ni dalili ya wazi kuwa hilo linajadiliwa kwenye sehemu za ibada. Hebu jamani tuilee na kuitunza amani yetu na tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa.

Mar 17, 2011

PESA ZA BANDIA ZA KAMATWA MWANZA.

Kaimu kamanda mkuu wa jeshi la polisi ndugu Deusdedith Msemeki akitoa taarifa za pesa chafu kwenyemzunguko wa fedha.Kamanda huyo alisema kiasi cha shilingi za kitanzania milioni kumi na nane lakisita na hamsini na tano elufu ambazo zimekusanywa kutoka maeneo mbalimbali. Akiendelea kutoa taarifa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na pesa hizo za bandia kwani zenyewe ni nene kidogo kuliko zile noti halali.Njia nyingine ya kuzitambua ni kuwa hata kama ni mpya noti bandia huchoka kwa kupauka haraka sana, na endapo pesa hizi ziko kwenye mabulungutu(bundles) zina tabia ya kufanana namba, kama ni AB......99 au 100 basi noti karibu zote zitafanana namba hizo.Pia kamanda ameelezea kuwa pesa hizi husambazwa kwa kufikishwa kwenye maeneo ya watu wengi kama minadani,sokoni,kwenye magari hasa daladala na hata benki pia.Hivyo aliwataka wananchi kuwa makini na fedha za bandia bila kuwataja watengenezaji na wasambazaji au kuwa wametiwa mbaroni au la.Hata hivyo amesema wanashughulika na pia kuzijulisha mamlaka kwa hatua zaidi.Mawazo yangu binafsi ni kuwa kama imewezekana kwa noti halali kurudufiwa kwa wingi ambapo hili limekuwa tatizo tangu pale tu pesa mpya zilipoingia tu kwenye mzunguko ni vema serikali ingeziondoa pesa hizi mpya kwenye mzunguko wa fedha. Kwakuwa pesa mpya ni rahisi sana kutengenezwa na watu wasio waaminifu, pesa hizi ziondolewe na zile za zamani ziendelee.Kwani kuacha mtindo huu kuendelea kutauangusha kabisa uchumi wetu kwa kuwa na mipesa mingi sana kwenye mzunguko ambapo hata kamanda amekiri kuwa benki pia pesa chafu hupita kwa mabeki teller wasio waaminifu.

PINDA OMBA MSAMAHA KWA MAGUFULI!

Wiki chache zilizopita waziri mkuu Mh.Pinda alipokuwa ziarani mkoani Kagera alitoa kauli ya kumdhalilisha waziri wa barabara Mh.Magufuli.Kauli ya Mh.Pinda ilikuwa ya kusitisha bomoabomoa kwenye hifadhi ya barabara kuu sanjari na matangazo makubwa ya biashara,ambapo hii ilikuwa ni kauli ya kitendaji ya waziri mwenye dhamana. Kama mh.Pinda aliona ni vyema zoezi hili kusitishwa ni bora angewasiliana na waziri husika na kukubaliana kwanza,kuliko kusimama hadharani na kutoa maamuzi kama hayo.Hadi sasa kuna tetesi kuwa waziri Magufuli ameandika barua ya kujiudhuru wadhifa wake huo kwa Rais Kikwete.Kama ni kweli basi upepo wa kisiasa utabadilika tena baada ya kutulia kwa muda na hasa baada ya kuibuka kwa suala la dawa ya kuponya magonjwa sugu kule Loliondo. Kweli hata mimi binafsi ninajisikia vibaya sana kwa uamuzi huu kwani kwamfano hapa Mwanza mabango yote makubwa yalikuwa yamebanduliwa na kusubiri tu kung'olewa kwa kuwa tayari yalikuwa na alama ya 'x' lakini cha kushangaza baada ya amri hiyo ya Magufuli mabango yale yamebandikwa tena,huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na hata kama ni mimi waziri ningejiudhuru.Ili kuondoa ombwe hili mapema Mh.Pinda aombe radhi kwa Mh.Magufuli.

Mar 6, 2011

'AU' YAPATA HASARA SOMALIA.

Majeshi ya African Uniun yanayoisaidia serikali dhaifu ya Somalia yamepata hasara kubwa baada ya kupoteza wanajeshi wapatao themanini.Majeshi hayo yanayoundwa na wanajeshi wengi kutoka Uganda na Rwanda yamekuwa Somalia kwa muda sasa ili kuipa serikali nguvu.lkumbukwe kuwa Somalia ilikuwa kwenye vita vya kikoo kwa muda mrefu hadi pale ilipoundwa serikali ya mpito ambayo ilikuwa ikifanyia shughuli zake nchini Kenya.Yote haya ni kuwa mabwana wa vita walitetemesha nchi hiyo na vikosi vingi vilivyotumwa huko vilishindwa.Baada ya umoja wa mataifa kushindwa kuleta amani nchini Somalia,kikaibuka kikundi cha kiislam ambacho kilitangaza Jihad dhidi ya mabwana wa kivita.Hatimaye mabwana wa vita walishindwa vita na Somalia kuwa yenye amani ambapo iliundwa serikali chini ya mahakama za kiislam na Amani kudumu kwa miezi sita.Mahakama hizi ziliweza kudhibiti hali ya amani ya nchi hadi pale Ethiopia ilipoingilia kati na kuishambulia Somalia wakiungwa mkono na wamarekani kwa kupewa vifaa na makomandoo ili kuiangamiza amani chini ya mahakama za kiislam mnamo mwaka 2006.Waziri mkuu wa Ethiopia Meresy Zenawi aliishambulia Somalia kwa kisingizio chakuwa mahakama za kiislam zinataka kutawala hadi Ethiopia,ikawa chanzo kipya cha mapigano nchini Somalia.Mapigano yalikuwa makali hadi majeshi ya kiislam yalipoamua kuondoka mjini kwa kuwa raia wengi walikuwa wanakufa.Vijana wa Kisomali waliamua kujiunga na kuunda kikundi chenye nguvu cha Al-shabab ambacho hadi sasa kiko kwenye mapambano makali na majeshi ya AU.Hivyo hii iko wazi kuwa umoja wa mataifa na umoja wa Afrika umeshindwa kuleta amani nchini somalia.Laiti kama mahakama za kiislam zingeliendelea kuidhibiti nchi basi amani Somalia ingekuwepo hadi leo kwani waliweza kudhibiti nidhamu.Wamarekani walichangia kwa madai ya kuwa ugaidi utatia mizizi pembe ya Afrika.Visingizio hivi ndivyo hadi leo vinasababisha hakuna amani pembe ya Afrika.

Mar 3, 2011

CHADEMA FUTENI KAULI YENU.

Kauli ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ya hivi karibuni jijini Mwanza huenda yakazua hatari kwa nchi na uvunjifu wa amani.Kauli hiyo ambayo ilikuwa kuwahamasisha mamia ya waandamanaji waliokuwa wamefulika katika uwanja wa Furahisha kwa kuwauliza kama wako tayari kwa maandamano kama ya Misri na Tunisia na kazi hii ikifanywa na mwenyekiti wa chama Mh.Freeman Mbowe "mkotayari kuandamana kama Misri na Tunisia?" watu wakaitika "tuko tayariii!" na haya yakifanyika maratatu ili kuhakikisha kama kweli watu wameridhia.Kama katika mikutano yote ya CHADEMA itakuwa hivi basi matarajio ni kuwa baada ya hapo huenda chama kikatoa tamko la maandamano nchi nzima,baada ya kazi ya kuwahamasisha raia.Endapo yatafanyika maandamano hayo ya kuipinga na kuifukuza serikali madarakani huenda yakaleta maafa kwa raia kwani sidhani kama serikali itakubaliana na hali hiyo.Vurugu zitasababisha uchumi kuparanganyika na watakaoumia zaidi ni watu wa hali za chini zaidi,kwani biashara ndogondogo hazitakuwepo na uharibifu wa mali kutokea.Vurugu zitakapoendelea watu watauana kutokana na visa tofautitofauti na kisingizio cha vurugu za kisiasa kutumika. Hadi sasa vijana wamehamasika kwa kiasi kikubwa sana, na hii ni kwasababu hawajui madhara ya vurugu.Mfano wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana baada ya vurugu zilizofanyika jijini Mwanza ambazo zilidhibitiwa mapema, baadhi ya vijana walisikika wakilalamika kuwa "hawa polisi wangesubiri giza liingie" nikajiuliza walitaka kufanya nini? lakini wakati huo ofisi ndogo za ccm zinaungua moto pale Nela.Kama wakati ule hakukuwa na kauli ya kiongozi wa chama aliyetamka kuwa tupinge matokeo na madhara yakaonekana vipi leo? Kauli hii ya chadema kwa sasa imekuwa mjadala wa nchi baada ya Rais Kikwete kulihutubia taifa na kuwaonya chadema kuacha kuhamasisha vurugu. Kwa kuwa katiba inaruhusu kuandamana basi chadema waandamane lakini si kuhamasisha vurugu na uvunjaji wa amani. Kilamtu amepewa uhuru na katiba wa kuongea na kutoa maoni yake lakini si kuvunja amani.Ombi langu kwa chadema,futeni kauli yenu ya kufanya maandamano ya kuifukuza serikali madarakani, kwani mpaka sasa wananchi wamegawanyika mapande mapande na wakati huohuo suala la udini likiwagawa raia,basi futeni kauli yenu na mwendeleze hoja za msingi ambazo zitatuunganisha Watanzania pamoja ili tuupige vita ufisadi kwa nguvu moja,kwani fisadi hana dini wala chama.