Mar 6, 2011

'AU' YAPATA HASARA SOMALIA.

Majeshi ya African Uniun yanayoisaidia serikali dhaifu ya Somalia yamepata hasara kubwa baada ya kupoteza wanajeshi wapatao themanini.Majeshi hayo yanayoundwa na wanajeshi wengi kutoka Uganda na Rwanda yamekuwa Somalia kwa muda sasa ili kuipa serikali nguvu.lkumbukwe kuwa Somalia ilikuwa kwenye vita vya kikoo kwa muda mrefu hadi pale ilipoundwa serikali ya mpito ambayo ilikuwa ikifanyia shughuli zake nchini Kenya.Yote haya ni kuwa mabwana wa vita walitetemesha nchi hiyo na vikosi vingi vilivyotumwa huko vilishindwa.Baada ya umoja wa mataifa kushindwa kuleta amani nchini Somalia,kikaibuka kikundi cha kiislam ambacho kilitangaza Jihad dhidi ya mabwana wa kivita.Hatimaye mabwana wa vita walishindwa vita na Somalia kuwa yenye amani ambapo iliundwa serikali chini ya mahakama za kiislam na Amani kudumu kwa miezi sita.Mahakama hizi ziliweza kudhibiti hali ya amani ya nchi hadi pale Ethiopia ilipoingilia kati na kuishambulia Somalia wakiungwa mkono na wamarekani kwa kupewa vifaa na makomandoo ili kuiangamiza amani chini ya mahakama za kiislam mnamo mwaka 2006.Waziri mkuu wa Ethiopia Meresy Zenawi aliishambulia Somalia kwa kisingizio chakuwa mahakama za kiislam zinataka kutawala hadi Ethiopia,ikawa chanzo kipya cha mapigano nchini Somalia.Mapigano yalikuwa makali hadi majeshi ya kiislam yalipoamua kuondoka mjini kwa kuwa raia wengi walikuwa wanakufa.Vijana wa Kisomali waliamua kujiunga na kuunda kikundi chenye nguvu cha Al-shabab ambacho hadi sasa kiko kwenye mapambano makali na majeshi ya AU.Hivyo hii iko wazi kuwa umoja wa mataifa na umoja wa Afrika umeshindwa kuleta amani nchini somalia.Laiti kama mahakama za kiislam zingeliendelea kuidhibiti nchi basi amani Somalia ingekuwepo hadi leo kwani waliweza kudhibiti nidhamu.Wamarekani walichangia kwa madai ya kuwa ugaidi utatia mizizi pembe ya Afrika.Visingizio hivi ndivyo hadi leo vinasababisha hakuna amani pembe ya Afrika.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.