Mar 3, 2011

CHADEMA FUTENI KAULI YENU.

Kauli ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ya hivi karibuni jijini Mwanza huenda yakazua hatari kwa nchi na uvunjifu wa amani.Kauli hiyo ambayo ilikuwa kuwahamasisha mamia ya waandamanaji waliokuwa wamefulika katika uwanja wa Furahisha kwa kuwauliza kama wako tayari kwa maandamano kama ya Misri na Tunisia na kazi hii ikifanywa na mwenyekiti wa chama Mh.Freeman Mbowe "mkotayari kuandamana kama Misri na Tunisia?" watu wakaitika "tuko tayariii!" na haya yakifanyika maratatu ili kuhakikisha kama kweli watu wameridhia.Kama katika mikutano yote ya CHADEMA itakuwa hivi basi matarajio ni kuwa baada ya hapo huenda chama kikatoa tamko la maandamano nchi nzima,baada ya kazi ya kuwahamasisha raia.Endapo yatafanyika maandamano hayo ya kuipinga na kuifukuza serikali madarakani huenda yakaleta maafa kwa raia kwani sidhani kama serikali itakubaliana na hali hiyo.Vurugu zitasababisha uchumi kuparanganyika na watakaoumia zaidi ni watu wa hali za chini zaidi,kwani biashara ndogondogo hazitakuwepo na uharibifu wa mali kutokea.Vurugu zitakapoendelea watu watauana kutokana na visa tofautitofauti na kisingizio cha vurugu za kisiasa kutumika. Hadi sasa vijana wamehamasika kwa kiasi kikubwa sana, na hii ni kwasababu hawajui madhara ya vurugu.Mfano wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana baada ya vurugu zilizofanyika jijini Mwanza ambazo zilidhibitiwa mapema, baadhi ya vijana walisikika wakilalamika kuwa "hawa polisi wangesubiri giza liingie" nikajiuliza walitaka kufanya nini? lakini wakati huo ofisi ndogo za ccm zinaungua moto pale Nela.Kama wakati ule hakukuwa na kauli ya kiongozi wa chama aliyetamka kuwa tupinge matokeo na madhara yakaonekana vipi leo? Kauli hii ya chadema kwa sasa imekuwa mjadala wa nchi baada ya Rais Kikwete kulihutubia taifa na kuwaonya chadema kuacha kuhamasisha vurugu. Kwa kuwa katiba inaruhusu kuandamana basi chadema waandamane lakini si kuhamasisha vurugu na uvunjaji wa amani. Kilamtu amepewa uhuru na katiba wa kuongea na kutoa maoni yake lakini si kuvunja amani.Ombi langu kwa chadema,futeni kauli yenu ya kufanya maandamano ya kuifukuza serikali madarakani, kwani mpaka sasa wananchi wamegawanyika mapande mapande na wakati huohuo suala la udini likiwagawa raia,basi futeni kauli yenu na mwendeleze hoja za msingi ambazo zitatuunganisha Watanzania pamoja ili tuupige vita ufisadi kwa nguvu moja,kwani fisadi hana dini wala chama.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.