Mar 21, 2011

DR.KIKWETE JIBU HOJA YA DR.SLAA.

Dr.Slaa mara kwa mara amekuwa akimtaja Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete katika kashfa za ufisadi. Katika ile the list of shame Rais kikwete alitajwa,na kutajwa huku kunatajwa hadharani kweupe lakini Rais Kikwete alijibu tu kuwa yeye si mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans. Rais Kikwete amehusishwa pia na Kagoda ambayo imevuna mabilioni ya mipesa katika akauti ya madeni ya nje ya EPA. Dr.Slaa amekuwa na kiburi cha kusema na kutaja kwa ujasiri mkubwa sana majukwaani, lakini hadi sasa hajafikishwa mahakamani kama alivyoburuzwa Mchungaji Christopher Mtikila alipo mdhihaki Rais. Hoja kuu iliyopo hapa ili kuondoa wasiwasi kwetu sisi raia tunataka Dr.Wilbrod Slaa afikishwe mahakamani kwa kumhusisha Rais na ufisadi.Kushindwa kumpeleka au kumshtaki Dr.Slaa inamaanisha ni kweli Dr.Slaa anao ushahidi wa wazi juu ya vitendo vya ufisadi kwa Rais Kikwete. Sasa hamu na shauku yetu wananchi ni kuona mahakama inatikisika kwa Dr.Slaa kufikishwa mahakamani. Ukimya wa mamlaka ya nchi kukaa kimya inatupa wasiwasi sana na kuamini kuwa yote yasemwayo ni kweli.Mwisho,nasisitiza tena na tena Dr.Slaa afikishwe mahakamani, na hoja zake pia zijibiwe kuliko kukaa kimya.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.