Mar 17, 2011

PESA ZA BANDIA ZA KAMATWA MWANZA.

Kaimu kamanda mkuu wa jeshi la polisi ndugu Deusdedith Msemeki akitoa taarifa za pesa chafu kwenyemzunguko wa fedha.Kamanda huyo alisema kiasi cha shilingi za kitanzania milioni kumi na nane lakisita na hamsini na tano elufu ambazo zimekusanywa kutoka maeneo mbalimbali. Akiendelea kutoa taarifa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na pesa hizo za bandia kwani zenyewe ni nene kidogo kuliko zile noti halali.Njia nyingine ya kuzitambua ni kuwa hata kama ni mpya noti bandia huchoka kwa kupauka haraka sana, na endapo pesa hizi ziko kwenye mabulungutu(bundles) zina tabia ya kufanana namba, kama ni AB......99 au 100 basi noti karibu zote zitafanana namba hizo.Pia kamanda ameelezea kuwa pesa hizi husambazwa kwa kufikishwa kwenye maeneo ya watu wengi kama minadani,sokoni,kwenye magari hasa daladala na hata benki pia.Hivyo aliwataka wananchi kuwa makini na fedha za bandia bila kuwataja watengenezaji na wasambazaji au kuwa wametiwa mbaroni au la.Hata hivyo amesema wanashughulika na pia kuzijulisha mamlaka kwa hatua zaidi.Mawazo yangu binafsi ni kuwa kama imewezekana kwa noti halali kurudufiwa kwa wingi ambapo hili limekuwa tatizo tangu pale tu pesa mpya zilipoingia tu kwenye mzunguko ni vema serikali ingeziondoa pesa hizi mpya kwenye mzunguko wa fedha. Kwakuwa pesa mpya ni rahisi sana kutengenezwa na watu wasio waaminifu, pesa hizi ziondolewe na zile za zamani ziendelee.Kwani kuacha mtindo huu kuendelea kutauangusha kabisa uchumi wetu kwa kuwa na mipesa mingi sana kwenye mzunguko ambapo hata kamanda amekiri kuwa benki pia pesa chafu hupita kwa mabeki teller wasio waaminifu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.