Mar 17, 2011

PINDA OMBA MSAMAHA KWA MAGUFULI!

Wiki chache zilizopita waziri mkuu Mh.Pinda alipokuwa ziarani mkoani Kagera alitoa kauli ya kumdhalilisha waziri wa barabara Mh.Magufuli.Kauli ya Mh.Pinda ilikuwa ya kusitisha bomoabomoa kwenye hifadhi ya barabara kuu sanjari na matangazo makubwa ya biashara,ambapo hii ilikuwa ni kauli ya kitendaji ya waziri mwenye dhamana. Kama mh.Pinda aliona ni vyema zoezi hili kusitishwa ni bora angewasiliana na waziri husika na kukubaliana kwanza,kuliko kusimama hadharani na kutoa maamuzi kama hayo.Hadi sasa kuna tetesi kuwa waziri Magufuli ameandika barua ya kujiudhuru wadhifa wake huo kwa Rais Kikwete.Kama ni kweli basi upepo wa kisiasa utabadilika tena baada ya kutulia kwa muda na hasa baada ya kuibuka kwa suala la dawa ya kuponya magonjwa sugu kule Loliondo. Kweli hata mimi binafsi ninajisikia vibaya sana kwa uamuzi huu kwani kwamfano hapa Mwanza mabango yote makubwa yalikuwa yamebanduliwa na kusubiri tu kung'olewa kwa kuwa tayari yalikuwa na alama ya 'x' lakini cha kushangaza baada ya amri hiyo ya Magufuli mabango yale yamebandikwa tena,huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na hata kama ni mimi waziri ningejiudhuru.Ili kuondoa ombwe hili mapema Mh.Pinda aombe radhi kwa Mh.Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.