Mar 26, 2011

WIMBO HUU TBCtaifa HAPANA.

Wimbo wimbo unaotumiwa kama kidokezo cha hotuba za hayati Mwl.Nyeree TBCtaifa kwakweli ni upotoshaji mkubwa wa historia ya Tanganyika.Muda mrefu wimbo huu nimekuwa nikiutathmini na kuutafakari na kukosa majibu kwa siku nyingi lakini sasa hatimaye nimegundua kisa na mkasa wa haya yote. Wimbo unasema "...kama sio juhudi zako Nyerere na uhuru tungepata wapi...? Kama sio juhudi zako Nyerere na amani tungepata wapi...?" Hii ni sehemu ya wimbo huo na mashairi yake ndio yaliyosababisha leo niseme haya nitakayosema.1.Watunzi wa wimbo huu na walioleta wazo la wimbo na wapigaji wa wimbo wanalengo la kuipoteza historia yote ya wapigania uhuru na kuonesha kuwa juhudi zote na kazi yote ya uhuru kafanya nyerere pekee. 2.Lengo ni kuonesha kuwa Nyerere ndio mwasisi wa mwanzo na wa mwisho wa harakati za kupigania uhuru na kuonesha au kukiaminisha kizazi kipya na kijacho kuwa Nyerere ndiye shujaa pekee katika historia ya Tanganyika.3. Wale wote waliojitolea kwa mali zao pia kumpa dhamana Nyerere kuwa kiongozi katika chama ambacho hakukianzisha na ambacho kilikuwa na malengo wala hawatajwi wala kupewa sifa na kuthaminiwa kuwa ni watu muhimu katika historia ya nchi yetu.Vitabu vya historia pia vyafuata mkumbo huohuo wa kumsifu Nyerere.4.Wimbo huu unaopigwa TBCtaifa usimamishwe maramoja na kutafutwa wimbo au kutafutwa kidokezo mbadala ambacho kinawatambua au kutambua juhudi za waasisi wa harakati za uhuru.Kupindishwa kwa historia ya Tanganyika ni juhudi za makusudi za kundi fulani kutaka kuonesha kuwa kundi jingine halina mchango wala halikuwa na mchango wowote katika mbio za kusaka uhuru.Kumbuka kuwa wakati wengine wakihudhuria ibada pamoja na wakoloni kundi la pili lilihangaika kuusaka uhuru wa nchi hii. Kundi hilo lililokula sahani moja na wakoloni leo linaeneza chuki za kidini kwa kueneza nyaraka za siri kwenye nyumba za ibada.Wakati kundi moja likidharauliwa kundi jingine linajineemesha na mikataba mbalimbali pia kupata misaada. Naomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya watu wachache wenye tabia hii mbaya ambayo muda si mrefu italiangamiza taifa.Serikali iandae majina halisi ya wapambanaji wa harakati za uhuru wote pasipo kumbagua yeyote miongoni mwao.Historia sahihi ya Tanganyika iandikwe kwani kuna uongo mwingi unaowekwa au uliowekwa kwenye historia na mfano mdogo ni kama wimbo huu wa wosia wa mwl.Nyerere kwenye redio ya Taifa. Kizazi kijacho hakitaijua historia na mashujaa kwa kuwa hawatajwi hata maramoja na hata serikali nayo iko kimya. Kweli wimbo huu ni mwiba kwa historia na kizazi kipya hakitawajua mashujaa bali Nyerere pekee.

1 comment:

  1. Ni kweli kabisa. Makosa na marekebisho ya historia yetu hayapewi kipaumbele na vitabu vinanampaaza Mwalimu na kuwasahu wengine waliochangia katika uhuru wetu.

    ReplyDelete

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.