Apr 24, 2011

PASAKA NA UNAFIKI WA AMANI

Amani ni kitu cha muhimu sana,yaani katika ngazi tofauti au ngazi mbalimbali kuanzia mtu binafsi,familia na taifa kwa ujumla.Kila mmoja wetu kama binadamu hupenda kuishi kwa amani bila kukwaruzwa kwa jambo lolote.Tatizo lililopo kwenye amani ni unafiki wa baadhi ya wanadamu ambapo wao huipenda amani na kujivunia kwayo lakini wao hawapendi wengine kuishi katika amani na pia hufurahi wanapoona jirani hana amani,watu hawa pia hutafuta nafasi za kuchokonoa amani za wengine hivyo kuleta kutokuelewana na hatimaye amani kupotea kabisa. Wiki hii tumeshuhudia na wengine kushiriki katika ibada na mikesha ya pasaka ambapo hotuba juu ya amani zilitawala. Kweli ilikuwa ni muhimu kwa mahubiri hayo kutawaliwa na kilio cha amani kutokana na umuhimu wa amani lakini,kwanini amani inaonekana kutoweka nchini? Je,ni kinanani wako nyuma ya moto huu mbaya? Je,ni viongozi wa dini au wa kisiasa? Jibu ni kuwa viongozi wa dini wenyewe na pia kwa kuwatumia wanasiasa ndio wamekuwa chanzo cha mvurugiko wa amani.Kama nchi ina makundi katika jamii na hasa moja likapewa nguvu na jingine kunyanyaswa! Hapo amani karibu ipo kutoweka. Viashiria vya kuvunjika amani Tanzania vipo wazi kabisa na vipo katika mtazamo wa kisiasa zaidi kwa wale wasiotambua,lakini mtafaruku huu uko wazi kuwa ni wakidini japo wasioona watapinga kwa nguvu. Kwa mfuatiliaji wa mambo yeye tayari ameng'amua mapema dalili zote.Vita iliyopo sio ya ccm na chadema bali ya Waislam na wakristo kwa sura ya kisiasa zaidi. Ndugu msomaji utakubaliana namimi kuwa makongamano ya Waislam yamefunua dhulma nyingi dhidi ya Waislam na hadi kulalamikiwa kuwa ni hatari eti kwasababu yanaelezea halihalisi ya Waislam nchini. Imefikia hatua vyombo vya habari vya Waislam kutishiwa kufungwa hasa gazeti la An-nur na radio Imani inayotangaza kutokea mjini Morogoro. Matusi na kejeli kutoka kwa vyombo vya habari hasa magazeti ambayo mengi yanamilikiwa na wakristo imekuwa ni kawaida,pia mtandao wa jamiiforum umekuwa chanzo cha kusambaza sumu ya udini nchini na mgawanyiko wa itikadi. Lengo langu kuu ni kuzitazama hotuba za pasaka kwa ujumla,lakini hebu tukumbuke nyuma kidogo ambapo mauaji ya Mwembechai,Zanzibar na Arusha na tulinganishe halafu tazama mwenendo wa katiba mpya kisha chukua hamasa za chadema kwa wananchi na wanafunzi wa elimu ya juu kisha uone.Rudi nyuma tazama mjadala wa mahakama ya kadhi Tanzania na lile la Tanzania kujiunga na OIC ambapo vitu hivi vilisababisha viongozi wa kidini kusema "damu itamwagika endapo serikali itaiingiza nchi OIC na kuwapa mahakama za kadhi Waislam".Mwerevu anajua na kutambua hatari tuliyonayo inatokea upande gani.Kumbuka tena vurugu za Arusha ambapo viongozi wa chadema walisema "tutahakikisha nchi haitawaliki".Maneno haya ni mazito sana! Lakini je,viongozi wa dini waliyagusia kwa uzito wake? Au walirashiarashia? Dr.Wilbroad Peter Slaa yeye ni Padri na kuingia katika siasa hizi yeye na chama chake wana agenda ya siri! Na hili hakuna kiongozi wa dini yeyote anayeweza kulizungumzia kwani huyu ni mwakilishi wao,badala ya kumkemea wao wanamtetea! Sasa kilio cha hotuba za pasaka kuhusu amani ni Unafiki mtupu kwani wahubiri wanajua tatizo lilipo na hawaoni haja ya kulitatua kwa malengo yao wanayoyajua. Hotuba au mahubiri na yaliyonyoyoni mwa wahubiri ni vitu viwili tofauti kabisa. Twende Rwanda kwenye mauaji ya kimbali,kule nako ilikuwa kama kwetu ambapo kwenye ibada tunahubiriwa amani na upendo lakini mwisho wa siku wahubiri ndio walikuwa washiriki wakubwa wa mauaji ya kimbali(halaiki) nchini humo. Kama kweli hotuba hizo zina dhamira ya kweli kutaka amani ya nchi basi wangeomba viongozi wa dini wote wawekwe pamoja na serikali na pia wale wakisiasa wakalishwe chini ili nyufa zizibwe la sivyo tutaishia kwenye dimbwi la damu. Ama kwa hakika kanisa na viongozi wake ndio wanao hatarisha amani yetu kwa kuandika nyaraka za kuligawa taifa kwa misingi ya dini,mfano mzuri ni nyaraka za kuelekea uchaguzi ambapo nyaraka hizo ziliandaliwa ili wakristo wamchague mgombea aliye chaguo la kanisa,kweli hii ni hatari sana! Kama wao ndio wanaoshabikia vitendo vya uvunjifu wa amani basi kweli msisitizo wa amani ni UNAFIKI uliowazi tena ni unafiki mweupe usio na doa. Napenda nichukue nafasi hii kumkumbusha Rais Jakaya M. Kikwete juu ya ahadi ya kukutana na viongozi wa dini mara kwa mara kwani huu ndio wakati muafaka ambapo nchi inatetemeka kabla ya kuanguka na kuvunjika vipandevipande.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.