Apr 26, 2011

KWA SIRI HII, MUUNGANO HAUVUNJIKI NG'O!

Leo tarehe 26 tunasherehekea miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe rasmi zinaadhimishwa katika uwanja wa Amani Zanzibar na mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho kikwete. Mengi yanasemwa kuhusu huu muungano wa Jamhuri ya Tanzania lakini wengi wao wanakwepa kuusema ule ukweli unaotakiwa kusemwa. Naomba ni mnukuu Mh.mama Anna Komu alipokuwa anahojiwa na TBC1 "wananchi wa Zanzibar hawakushilikishwa wakati wa kufanya muungano,ila walikaa viongozi na kukubaliana".Wazanzibar wamelalamika siku nyingi juu ya Muungano huu hadi ukazuka msamiati wa "kero za Muungano".Zimeundwa kamati mbalimbali kushughulikia muungano lakini bado kamati hizi bado hatujaona matunda yake kwa maana ya kuziondosha kero za muungano. Je,Muungano waweza kuvunjika? Jibu lake ni HAPANA. Kwanza nianzie nyuma kidogo ili nikuoneshe ni kwanini Muungano hata kwa dawa hauvunjiki yaani hata Wazanzibar walie machozi ya damu. Tanganyika ilitawaliwa awamu ya kwanza na Wajerumani kisha wakaja Waingereza,nyakati zote hizi wazee wetu walipambana kudai uhuru wa Tanganyika na hatimaye mwaka 1961 uhuru ukapatikana.Wakati wa mbio za kudai uhuru Mwl.Nyerere ndiye pewa jukumu na wazee ili aende kwenye Jumba la mabwanyenye akadai uhuru. Maombi ya uhuru yakakubaliwa chini ya masharti.Masharti hayo kwenye mkataba ambao ulikuwa siri kati ya nchi tawaliwa na watawala,hadi sasa hakuna ajuaye Mwl.Nyerere alisaini masharti gani ili tupewe uhuru ambayo yeye alikubaliana nayo.Baada ya uhuru Mwl.Nyerere alitia fitina na kuuvunja umoja wa Waislam Afrika Mashariki(EAMWAS) na kuwafukuza mashekhe nchini na wengine kuwaweka kizuizini.Baada ya kuivunja EAMWAS aliwaundia Waislam BAKWATA ilikuwa chini ya uangalizi wa serikali yake. Hapa nia na madhumuni ilikuwa kuwavunja nguvu Waislam,kwa kuwa tayari walikuwa na nguvu kubwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii.Hivyo waislam waligawanywa na wakagawanyika pia nguvu ikaisha kwa kuwa mashekhe walifukuzwa nchina na wengine kizuizini, hivyo harakati za uislam kusonga mbele zikafifia na mahala pengine kufa kabisa,hii ilitokana na hofu kubwa waliyokuwa nayo wanaharakati baada ya kushuhudia yaliyotokea kwa ndugu zao. Kwa upande wa Zanzibar,Zanzibar yenyewe ilitawaliwa na Sultan kutoka Oman pia baada yake walitawala watoto wake mpaka pale waingereza walipo kuja kuleta fitna baina ya watawala ambao ni watoto wa Sultan.Waingereza walimpatia silaha mtoto mmoja wa Sultan ili apambane na nduguye juu ya madaraka ya kuitawala Zanzibar,baada ya mapambano aliyekuwa madarakani alikimbia na kumwachia mshindi ambaye ni kibaraka wa Waingereza. Kipindi chote cha utawala wa Sultan hadi kwa watoto wake wote wawili Uislam Zanzibar ulinawili na kuwa na nguvu kubwa.Uislam ulikuwa umeenea maeneo yote ya pwani na kuanza kuingia bara kwa kasi.Baada ya uhuru wa Zanzibar mchakato wa muungano ulianza haraka sana ambapo 1964 Tanzania ilizaliwa.Agenda kuu ya siri ilikuwa kuudhibiti Uislam usienee bara kwa nguvu kwani EAMWAS ilikuwa tayari imekufa. Mambo yote ya muungano huamuliwa Dodoma,Zanzibar ikawa inachaguliwa marafiki tena wale ambao Dodoma iliwataka. Kumbuka Zanzibar ilipotaka kujiunga na OIC haraka Dodoma ilikataa na kusema hilo ni jambo la muungano na Zanzibar sio nchi na madai hayo ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano. Hofu iliyopo nikuwa Zanzibar ikijitenga Uislam utapata nguvu na kuhatarisha ustawi wa Ukristo Afrika mashariki hivyo lazima Zanzibar idhibitiwe kwa vyovyote vile hata kama wananchi hawataki.Wote waliohoji muungano hawakosalama na mifano tunaiona wazi,Abdu Jumbe alihoji,akaitwa Dodoma na kuvuliwa nyadhifa zake zote na kuishia kizuizini na historia yake ikafutika.CUF na sera yao ya "tukipata madaraka tunavunja muungano" wakatiwa lupango kina Duni Haji na kupewa kesi ya uhaini. Pia inasemekana kuwa hata Karume aliuawa baada ya kuazimia kuvunja Muungano baada ya kujua siri iliyopo. Wazanzibar sasa wanalilia muungano kuvunjika na hili limedhibitika hivi karibuni ambapo wananchi walichanachana muswada wa katiba mpya ambao haukutaka Muungano kujadiliwa,kutokutaka muungano kujadiliwa kuna maana kuwa mambo yalivyo yaendelee kuwa hivyohivyo na asiyetaka ashughulikiwe. Ustawi wa ukristo nchini unategemea nguvu ya Uislam nchini kwani mambo yanayotokea hivisasa yanadhibitisha. Kumbuka uchaguzi wa mwaka2000 ambapo ilikuwa dhahiri CUF Zanzibar ilishinda ila kutokana na sera yake ya kuuvunja muungano CUF ikakosa madaraka na kuwalazimu wananchi wa Zanzibar kuingia barabarani ambapo walisagwasagwa kwa mkono wa chuma,mauaji makubwa yalitokea na kwa mujibu wa DotchWelle idhaa ya kiswahili ambapo mwanamke mmoja alikuwa akihojiwa na kwa uchungu alisema "huko mtaani maiti zimezagaa,kwakusia watu zaidi ya 80 wamekufa,kwani askari wanapiga risasi hovyo na kunawengine wanawekwa kwenye makarandinga.Na kunahabari kuwa kuna mashua ilikuwa na raia wakikimbilia Kenya wamefuatwa kwa helkopta na kupigwa kombora". Hata hivyo habari za helkopta zilikanushwa.Kwa siri hii kuu,Muungano hauvunjiki ng'o!

No comments:

Post a Comment

Tafadhali toa maoni yenye kujenga na sikuboa.Lugha chafu zisitumike.